

MIKONO YA KIHAMU YA FARHAN JR
TAJIRI GSM, ONE THING ABOUT FOOTBALL, IS NOT FOOTBALL
Aliwahi kuulizwa Kocha Sir Alex Ferguson, ni nani mtu muhimu sana kwako kwenye setup nzima ya Manchester United? Nae akasema kiwepesi sana, ni DAVID GILL
Akaendelea kusema "Listen to me Kids, one thing about football is not about football" akiwaambia Wanafunzi kutoka Chuo cha Havard kitivo cha Biashara
Kwa kifupi Fergie alimaanisha kitu kimoja kuhusu mpira, huwa wala hakihusu mpira! Yani mafanikio ya Manchester United yalianzia kwenye eneo la viongozi, kuanzia Matajiri, Bodi na Mtendaji Mkuu David Gill
Naona Tajiri GSM anavyopambana sana kuirejesha Yanga Afrika kwenye ramani, haswa zaidi kuwekeza uwanjani kwenye kikosi hii process inaitwa INSTANT SUCCESS! Wanachojaribu kukifanya Yanga kiliwahi kufanywa na Chelsea (Tutaongea siku)
Lakini naomba nimwambie kitu Tajiri GSM kwa elimu yangu ndogo sana, pale Chelsea walikuwa na Michael Emenalo akipambania mipango (Plans implementor), Roman aliweka pesa ila yeye ndie alizigeuza pesa kuwa Mataji, alikuwa Mtendaji mzuri sana
Nachokiona kwa Wananchi, sio uwanjani bali ni eneo kubwa la utawala! Wanapaswa kuweka nguvu kubwa kujenga timu kali ya Utawala (Executive) hawa watageuza pesa zake kuwa Mataji pale Yanga
Naomba nimpe pia mfano mwingine Tajiri GSM, wale Waarabu wa Manchester City nchini ya Sheikh Mansour Bin Zayed waliwahi kumuhitaji Pep Guardiola wakati yupo mapumziko ya mwaka mzima Jijini New York
Guardiola aliwaambia mna pesa nyingi sana ila bado hamna ushindi! Akampa majina mawili Mwenyekiti wa City, Khaldoon Mubarak, alimpa jina la Ferran Soriano na Txiki Berigistein! Hawa ni miamba na ndio walikuwa mihimili ya FC Barcelona
Txiki sasa yupo City na ndie Director of Football na Soriano sasa yupo City ndie Mtendaji Mkuu wa Klabu, ndipo hapo Pep akasogea baadae kujiunga na City akiamini tayari timu imetimia na wanaweza kufanya kitu kikubwa barani Ulaya
Tajiri GSM umemaliza kusajili sasa pambana kusaka Watawala, unda timu ya ushindi kuanzia ofisini na Yanga itarejea pale unapotaka! Kinachokutokea ndicho kinawatokea Arsenal, wana timu ya Viongozi ambao hawana Uzoefu