Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210831-135926_Instagram.jpg
 
| TANZANIA YATOA WAAMUZI WANNE LIGI YA MABINGWA
.
Marefa wanne wa Tanzania wamepangwa kuchezesha mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Mogadishu City ya Somalia na APR ya Rwanda utakaochezwa Septemba 12 huko Djibouti.
.
Ramadhan Kayoko ndiye atakuwa mwamuzi wa kati ambapo atasaidiwa na Frank Komba na Soud Lila huku refa wa akiba akiwa ni Mfaume Ali Nassoro.
.
Taratibu tunapiga hatua
@ramadhan_kayoko
kombafrank @soudlila @AliNasoro.

Screenshot_20210831-140105_Instagram.jpg
 
Mwanzo wa Messi PSG wamkuna Pochettino
.
Mauricio Pochettino amebainisha namna gani mchango wa Lionel Messi tayari umekuwa na manufaa kwa wachezaji wenzake wa Paris Saint-Germain baada ya nyota huyo mpya kucheza mchezo wake wa kwanza na klabu hiyo.
.
"Ameleta kitu kikubwa kwa timu. Ni muhimu kuanza vizuri kwa upande wake,"
.
"Alikuwa na furaha na alionekana kujichanganya vizuri na kundi la wachezaji wenzake. Lilikuwa jambo zuri na kwa hakika naamini mambo mazuri zaidi yataendelea.
.
"Kukaribishwa kwake kulikuwa kuzuri zaidi na tuliona mashabiki wa timu zote walionekana kuwa nashauku kubwa ya kutaka kumwona hasa wale wa Reims. Messi alikuwa na furaha kubwa.”
Screenshot_20210831-140235_Instagram.jpg
 
OFFICIAL | Beki Ruben Dias amesaini mkataba mpya wa miaka sita na klabu ya Manchester City.
.
Msimu uliopita, Dias alicheza mechi 50 wakati City ilinyakua taji lao la tano la Ligi Kuu, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 akitajwa kuwa Mchezaji bora wa msimu na Mwanasoka wa Chama cha Waandishi wa Soka wa Mwaka.
Screenshot_20210831-140445_Instagram.jpg
 
𝐎𝐁𝐑𝐈𝐆𝐀𝐃𝐎 𝐘𝐔𝐒𝐔𝐏𝐇 𝐌𝐇𝐈𝐋𝐔

AGREED
KAGERA SUGARSIMBA SC

Tumefikia makubaliano ya pande zote mbili (Kagera Sugar FC na Simba Sc) juu ya uhamisho wa aliyekuwa mchezaji wetu Nyota Yusuph Valentine Mhilu kwa Dau la Tsh.40M.

Yusuph Mhilu alisaini kandarasi ya miaka Miwili kuitumikia Kagera Sugar Football Club Mwaka Jana 2020. Hivyo uhamisho huu wa Yusuph Mhilu kwenda Simba ni Uhamisho ambao umehusisha kuvunja Mkataba wake wa Mwaka mmoja uliosalia ndani ya Klabu ya Kagera Sugar #wanankurukumbi

Tunamtakia kila la Kheri huko aendako na Mungu amsimamie katika kukiendeleza kipaji chake
Screenshot_20210831-171804_Instagram%20Lite.jpg
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba Leo August 31,2021 ametia saini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kieletroniki za Kutuma na Kutoa Fedha za Mwaka 2021 na kupunguza viwango vya tozo za miamala kwa 30% huu ukiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia ambaye alielekeza tozo zipitiwe upya baada ya kusikia kilio cha Wananchi kuhusu tozo hizo.

Serikali pia imefanya majadiliano na watoa huduma za simu ambao na wameridhia kupunguza viwango vya tozo wanazotoza katika miamala ya kutuma na kutoa fedha kati ya mtandao na mtandao mwingine kwa 10%.

Viwango vilivyopunguzwa vitatangazwa rasmi kwa Tangazo la Serikali kesho September 01,2021 ambapo Serikali imesema inaamini uamuzi huo utatoa nafuu kwa Wananchi na kuiwezesha Serikali kupata fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyokusudiwa wakati tozo hizo ziliporidhiwa na kupitishwa na Bunge la Bajeti la Mwaka 2021/2022.
Screenshot_20210831-202556_Instagram.jpg
 
Kundi la Taliban limesherehekea kuishinda Marekani na kuchukua mamlaka kamili leo Jumanne baada ya vikosi vya mwisho vya Marekani kuondoka nchini Afghanistan na kumaliza vita vya miongo miwili.

Wapiganaji wa Taliban waliokuwa na furaha waliingia katika uwanja wa ndege wa Kabul na kupiga risasi angani kama ishara ya kuchukua madaraka kamili.

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid amewaambia waandishi habari kuwa ushindi wa kundi hilo unafaa kuwa funzo kwa wavamizi wengine.

Vita virefu zaidi vya Marekani vilikamilika Jumatatu usiku baada ya wanajeshi wake kuondoka kabisa katika uwanja wa ndege wa Kabul, ambapo walikuwa wakisimamia oparesheni za kuwahamisha watu.

Zaidi ya Watu 123,000 wameondoka nchini humo kwa kuhofia utawala wa Taliban.
Screenshot_20210831-203137_Instagram.jpg
 
Miongoni mwa video kutoka Afghanistan zilizogusa hisia kwa saa 24 zilizopita ni hii ya Mtangazaji wa Afghan TV kuvamiwa akiwa Live Studio na Wapiganaji wa Taliban wakiwa na bunduki na kumshinikiza kuwamwagia sifa na kuwatangazia Wananchi kuwa wao ni Watu wema.

Mtangazaji akiwa na hofu alisikika akiwataka Wananchi kushirikiana na Taliban na wasiogope ambapo baadae alimuhoji mmoja wa Wapiganaji hao huku wengine wakiwa wamemzunguka na Bunduki zao.
Screenshot_20210831-203347_Instagram.jpg
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu (Mahakama ya Mafisadi), inatarajia kutoa uamuzi Septemba 1, 2021 kama ina mamlaka ya kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake ama lah.

Kesi hiyo imetajwa leo mbele ya Jaji Luvanda ambapo upande wa washitakiwa ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala uliibua hoja ya kutaka kesi hiyo ifutwe kutokana na Mahakama ya Mafisadi kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za Ugaidi.

Hata hivyo, upande wa Jamhuri ulipinga hoja hiyo na kusema Mahakama hiyo ina mamlaka.
Screenshot_20210831-203531_Instagram.jpg
 
“Kuhusu Gwajima sisi hapa hatujamshitaki kama Askofu, tumemshtaki kama Mbunge Gwajima, habari za Uaskofu wake ni hukohuko, unaweza ukawa Askofu halafu kama wenzako hawaelewi Dini sio hivyo hayo ni macho ya Makengeza Watu ni Waumini sana”

“Mimi ni Mzee wa Kanisa la Anglikana wa miaka mingi, ni nafasi ya Mshauri wa Askofu, nimeshakwenda Nigeria kwa TB Joshua, nimeenda Makao Makuu ya Kanisa langu, Uyahudi nimekwenda mara nne, nimeenda kwenye Kijiji cha Yesu, Galilaya yote ile nilitembea naijua”

“Nimefika Nazareth, mara ya mwisho nimeenda na Mwalimu Mwakasege, tunatamba sisi?, sasa ukiwa Askofu utudanganye sisi?, Dini tunaijua, mnavyokwenda sio kutumia platform ya Dini kila Jumapili kuhamasisha “Mtusikilize, mtasikia mabomu kesho” Waziri wa Mambo ya Ndani uko hapa, Serikali mko hapa hii haiwezi kwenda hivi” ——— Spika Ndugai.
Screenshot_20210831-203853_Instagram.jpg
 
Baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge Emmanuel Mwakasaka kutoa ripoti ya Kamati hiyo kuhusu hatia walizokutwa nazo Wabunge Jerry Silaa na Josephat Gwajima, Spika Job Ndugai amemtoa Bungeni Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa.

“Gwajima hayupo, Silaa yupo sasa naomba Silaa utoke nje tutaonana January,2022 na Sajenti naomba mtoke nae nje ya viunga vya Bunge na katika kipindi hiki ambacho wamesimamishwa hawatoruhusiwa kukanyaga maeneo ya Bunge isipokuwa kwa ridhaa ya Spika na watapata nusu ya mshahara na nusu ya mambo mengine ambayo watastahili kuyapata hivyo ndivyo kanuni zinavyosema” ———Ndugai
Screenshot_20210831-210126_Instagram.jpg
 
Steven Gerrard atema nyongo kwa Ronaldo:
.
"Nadhani Cristiano Ronaldo hatallfanya makubwa katika Ligi Kuu ya England kama alivyofanya zamani. Nadhani aliomba kuondoka Juventus ili kurudisha vichwa vya habari kwake. Hii ni kwa sababu macho yote yalikuwa kwa Messi tangu siku aliyoshinda ubingwa ws Copa America na kuhamia Paris Saint-Germain.
.
"Huu ni mkakati tu wa kujibrand yeye na wakala wake kwa sababu wanajua akishapoteza mvuto kwenye vyombo vya habari, pia itaathiri nafasi yake ya kushinda Ballon d'Or , ambayo nadhani bado hana nafasi ya kushinda kwa mwaka huu. ”


Gerrard tuache kidogo na Ronaldo wetu sio mtu wa kiki
Screenshot_20210831-210757_Instagram.jpg
 
| SAMATTA ROYAL ANTWERP
.
Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ametua leo, Jumanne huko Ubelgiji ikiwa ni siku ya mwisho ya usajili barani Ulaya kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kujiunga na Royal Antwerp akitokea Fenerbahce ya Uturuki.
.
Imeripotiwa kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania uhamisho wake umeigharimu Antwerp kitita cha Euro milion 4 ambazo ni zaidi ya Sh. 10.9 Bilioni.
.
Katika vita ya kuiwania saini yake,Antwerp imepigana vikumbo na klabu kadhaa ikiwemo Troyes na Montpellier za Ligi Kuu Ufaransa.
Screenshot_20210831-211019_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom