NABI: NIPENI MUDA BADO SIJAPATA MUUNGANIKO WA TIMU
.
Kocha mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi ametua nchini jana na kutamka kwamba bado hajapata muunganiko katika timu yake licha ya kuwa nchini Morocco kwenye maandalizi ya msimu mpya.
.
Akizungumza na waandishi wa habari, Nabi amesema; “Muunganiko wa timu bado, tunahitaji muda kama mwezi au miezi mitatu kwa sababu timu haijengwi kwa muda mfupi.
.
Wachezaji wote tuliowasajili ni wazuri kwa sababu tulikuwa tunawafuatilia, tukipata muda zaidi tutakuwa bora zaidi,” alisema Nabi.
.
Naye mshambuliaji Saido Ntibazonkiza alisema; “Kama kocha alivyosema muda ulikuwa mchache lakini tukiunganika vizuri tutakuwa bora zaidi, kikosi kipo vizuri.”