Mpaka sasa Barcelona wapo kwenye 95% ya mishahara, wanapambana kuona namna gani wataliingiza jina la Memphis Depay kwenye mfumo maana mshahara unaweza kuvuka hizo 5% zilizosalia
Rais Joan Laporta, alikuwa na mipango kadhaa kuokoa jahazi
-European Super League, imesalitiwa na waoga, wamebaki wao watatu tu
-Dili la mkopo wa CVC Media Partners halina maslahi litaiweka klabu kwenye hasara ya muda mrefu
Zimesalia njia mbili pekee hatarishi ambazo tunasubiri atachukua ipi
Mosi, kuuza sehemu ya haki za La Masia na majengo kadhaa ya klabu ili kubalance vitabu
Pili, kuuza baadhi ya wachezaji tegemezi ili kutunisha mfuko ambao ni Pedri, Frank De Jong yoyote kati yao, japo hii ni ngumu sana kufanyika
Tatu, ni Wachezaji kukubali kuendelea kupunguza mishahara yao ili kuisaidia klabu! Hii ndio njia inayojadiliwa zaidi mpaka sasa
Bado mapambano yanaendelea wakati LA LIGA inakaribia kuanza
BARCELONA wana hali ngumu sana