KUMBE KANE KESHAMALIZANA
.
Lisemwalo lipo Na kwenye hilo ni kwamba straika Harry Kane ameshamalizana na Manchester City juu ya makubaliano binafsi wakati huu akijiandaa kuachana na Tottenham Hotspur
.
Kane, 28, bado anafukuzia taji lake la kwanza kwenye maisha ya soka na jambo hilo ndilo linalotajwa kuwa sababu kubwa itakayomwondoa Spurs, mahali ambalo alizua utata siku za karibuni baada ya kukosekana mazoezini kwa wiki nzima.
.
Ripoti zinafichua kwamba mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy ambaye amekuwa akiweka ngumu kwenye kukubali kumuuza mshambuliaji huyo, sasa amelegeza msimamo wake na kwamba amekubali ofa ya Pauni milioni 120 pamoja na nyongeza nyingine ya Pauni 20 milioni ili kukamilisha dili hilo.
.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari, Ian McGarry amesema: “Harry Kane ni ameshakubaliana mambo binafsi na Man City na kinachosubiriwa ni Daniel Levy kukubali ada ya uhamisho.”