Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210809-064917_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20210809-065247_Opera%20Mini.jpg
 
Hizi ni picha mbalimbali za mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa vilevile Mbunge wa Jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa.

Kwandikwa amezikwa leo Agosti 9 kijijini kwao Butibu, Ushetu wilaya ya Kahama na Waziri Mkuu ameongoza Waombolezaji wengine kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Kwandikwa baada ya kupigiwa mizinga 17 na JWTZ kwa heshima ya Uwaziri wa Ulinzi.

RIPKwandikwa
Screenshot_20210809-182441_GBInsta.jpg
Screenshot_20210809-182526_GBInsta.jpg
Screenshot_20210809-182551_GBInsta.jpg
Screenshot_20210809-182607_GBInsta.jpg
Screenshot_20210809-182625_GBInsta.jpg
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imekubali ombi la Mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe la kumruhusu Mbowe kuhudhuria shauri lake la Kikatiba alilolifungua dhidi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Shauri hilo namba 21 la mwaka 2021 linasikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu John Mgeta, Steven Magoiga na Leila Mgonya ambapo litatajwa Agosti 30, 2021.

Katika kesi hiyo, Mbowe anapinga hatua ya kushtakiwa kwa kosa la ugaidi kimyakimya bila kumtaarifu kuhusiana na mashtaka hayo, huku akieleza maneno ya vitisho anayodai kupewa na Polisi.

Sambamba na madai hayo Mbowe anadai haki zake kukiukwa kwa kutokujulishwa na kupewa fursa ya kuwasilisha kuwajulisha Nduguz zake na Wakili wake, pia Mbowe anadai kuwa wakati alipokwa ameshikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay alikuwa akipokea kauli za kejeli na vitisho kutoka kwa Afisa wa Polisi.

Mbowe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakikmu Mkazi Kisutu, July 26, 2021 na kusomewa mashtaka ya ugaidi katika kesi aliyoungianishwa na washtakiwa wengine ambao walikuwa wameshapandishwa kizimbani tangu mwaka jana 2020.
Screenshot_20210809-182934_GBInsta.jpg
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ameaigiza Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kufanya kikao na Wadau ndani ya wiki moja na kuwapitisha katika marekebisho ya Kanuni ya Leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa Umma ya Mwaka 2003.

Bashungwa ametoa agizo hilo Dar es Salaam alipofanya kikao na Menejimenti ya Taasisi hiyo kufuatilia marekebisho ya Kanuni hiyo ambayo imefanyiwa marekebisho ya tozo katika maeneo mbalimbali ya biashara yanayotumia kazi za Muziki.

‘’Ndani ya wiki moja kuanzia leo muende kwa Wadau mkawapitishe katika marekebisho haya ili nao watoe maoni yao, tulikamilishe hili kwa haraka ikumbwe kuna maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwa tunatakiwa kugawa mirabaha mwezi Disemba ni lazima mkamilishe hili kwa haraka”———Bashungwa

Bashungwa ameitaka COSOTA kuhakikisha inazingatia maoni yote ya Wadau ili kuepuka migogoro wakati kanuni hizo zitakapoanza kutumika.

Kwa upande wake Mwanasheria wa COSOTA Lupakisyo Mwambinga katika wasilisho lake la marekebisho hayo ya Kanuni hizo alifafanua kuwa baadhi ya maeneo yamefanyiwa marekebisho kutokana gharama za tozo zake kuwa na kiwango cha chini kisichoendana na gharama za maisha ya sasa sababu ni tozo za muda mrefu.
Screenshot_20210809-183220_GBInsta.jpg
Screenshot_20210809-183237_GBInsta.jpg
 
Katika kuhakikisha kunakuwa na uharakishwaji wa uendeshwaji wa kesi zinazohusu mirathi, talaka na zile zinazohusu Watoto,Serikali inakamilisha ujenzi wa jengo la kisasa la mahakama katika eneo la Chang’ombe wilayani Temeke litakalokuwa maalumu kwa kuendeshea mashauri hayo.

Akikagua jengo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema kukamilika kwa jengo hilo kutakuwa ni suluhisho kwa mashauri hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakicheleweshwa kutokana na Mahakama nyingi kuwa na mashauri mengine tofauti.

‘’Takwimu zinaonesha kuwa Wilaya yetu ina idadi kubwa sana ya Watu na kuna wastani wa Watoto zaidi ya 100 wanaozaliwa kila siku, hii inapelekea kuwa na migogoro na kesi nyingi za mirathi, kesi za Watoto na hata talaka’’———Jokate

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Wilaya ya Temeke Ilvin Mugeta, amesema ujenzi wa Mahakama hiyo utasaidia kupunguza muda wa kumaliza shauri kutoka mwaka mmoja hadi miwili ya sasa mpaka miezi sita huku akisisitiza Wananchi kuitumia miundo mbinu ya Mahakama hiyo vizuri.

Jengo hilo litakuwa la kwanza la aina yake hapa nchini ambapo kutakuwa na Mahakama ya Mwanzo, Wilaya na Mahakama kuu ambapo zitakuwa ni maalumu kwa kusikiliza mashauri yanayohusu kesi za mirathi, talaka na Watoto na linatarajiwa kufunguliwa rasmi mwezi wa tisa mwaka huu na Rais Samia Suluhu Hassan.
Screenshot_20210809-183445_GBInsta.jpg
Screenshot_20210809-183539_GBInsta.jpg
Screenshot_20210809-183606_GBInsta.jpg
Screenshot_20210809-183622_GBInsta.jpg
 
Staa wa Soka na Mchezaji Mwandamizi wa Simba SC Jonas Mkude leo ameripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao 2021/2022 baada ya kuwa nje ya Timu kwa zaidi ya miezi miwili kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

June 07, 2021 Kamati ya Nidhamu ya Simba SC chini ya Mwenyekiti wake Selemani Kova iliahirisha hukumu ya tuhuma za utovu wa nidhamu kwa kiungo Jonas Mkude na kuagiza kuwa Mkude akapimwe ili kujua kwa nini ana makosa ya kujirudia.

Simba SC sasa inaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya na Wachezaji wamewasili leo kama Kocha wao Mkuu Didier Gomes alivyoagiza, inasemekana Simba SC itaweka kambi ya maandalizi nchini Morocco.
Screenshot_20210809-183927_GBInsta.jpg
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Kenani Laban Kihongosi amesema wanasikitishwa na matendo yanayofanywa na Mbunge Humprey Polepole kuhusu suala la chanjo, kwani Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameshasema Kwamba chanjo ni hiari na maamuzi yake lazima yaheshimiwe.

“Tunapenda kumwambia Mbunge Polepole kwamba awe na nidhamu na adabu kama aliyokuwa nayo wakati wa Utawala wa Awamu ya Tano, nidhamu ileile aiendeleze pia katika Utawala huu wa Awamu ya Sita Inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, mijadala yake kuhusu chanjo ni bora akakaa kimya kama haitaji kuchanja, lakini sio kujificha katika kivuli cha chanjo kuipinga Serikali”———Kihongosi

“Kamwe hatutovumilia utovu wowote wa nidhamu kwa Rais Samia na Serikali yake, sasa kuendelea kutengeneza maneno ya kejeli, dhihaka na mengine ya aina hiyo yanabeba mazingira yanayotia shaka dhamira yake aliyonayo kwa Mwenyekiti wetu na Rais wetu wa Tanzania, tunamtaka aache mara moja”———Kihongosi

“Chama cha Mapinduzi sio Chama cha harakati bali ni Chama kilichojijenga katika misingi ya kutii na kuheshimu Viongozi, hivyo jambo lolote la kupinga au kuendeleza mijadala ambayo Mwenyekiti wa CCM Taifa ameshaitolea maelekezo ni utovu wa nidhamu kwa Chama na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi”———Kihongosi

“Tunamuonya na tunamtaka aache mara moja kwani hatutakubali Kiongozi yoyote avunje heshima ya Rais Samia Suluhu Hassan au kupinga yale aliyoyaelekeza”———Kihongosi
Screenshot_20210809-184122_GBInsta.jpg
 
Muuguzi wa Zahanati ya Kisiwani na Dereva wa gari la kubebea Wagonjwa (ambulance) wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa Mkoani Kilimanjaro baada ya gari hilo kupinduka na kupoteza mwelekeo wakati wakimuwaisha Mgonjwa Hospitali ya Wilaya ya Same.

Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Simon Maigwa amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya kupasuka kwa tairi la upande wa kushoto ambalo amesema lilikua limechakaa na katika uchunguzi uchakavu huo ndio umeonekana ni chanzo.
Screenshot_20210809-184316_GBInsta.jpg
 
Ameandika Meneja wa Kipa Metacha Mnata, Jemedari Said

Rasmi sasa Yanga SC imeachana na golikipa wake namba moja Metacha Mnata.

Metacha amekabidhiwa barua yake ya kuwa huru leo mchana, baada ya kumaliza mkataba wake na Klabu hiyo. Alijiunga na Yanga SC mwaka 2019 akitokea Mbao FC ya Mwanza.
Screenshot_20210809-184523_GBInsta.jpg
 
Baada ya nchi mbalimbali kuchanja idadi kubwa ya watu wao chanjo ya corona, baadhi zimeanza kuweka masharti kwa wageni wanaoingia kuwa ni lazima wawe wamechanjwa dhidi ya virusi vya corona.

Nchi hizo sasa zimeanza kuweka masharti hayo kupitia baadhi ya mashirika ya ndege yanayobeba abiria, kuwa hawatakubali kumpokea raia yeyote ambaye hajachanjwa ili kudhibiti virusi hivyo kwenye nchi zao.

Hata hivyo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa ufafanuzi kuwa hakuna sharti la chanjo ya corona kwa wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.

Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Afya, Catherine Sungura amesema ni vema msafiri akauliza shirika la ndege analokwenda nalo pamoja na masharti ya nchi anayotembelea.

“Kwa zile nchi ambazo zinahitaji kipimo cha Covid-19 msafiri afanye kipimo hicho ndani ya saa 24 hadi 48 kabla ya kuanza safari.
Screenshot_20210809-184651_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom