Makapuku Forum

WACHEZAJI WAANZA KUREJEA MSIMBAZI

Wachezaji wa Simba PERFECT CHIKWENDE
na CLATOUS CHAMA
wamesharejea ncchini kama alivyoagiza kocha wa timu hiyo Didier Gomes ambaye anataka kuanza maandalizi ya msimu ujao.

Simba inatarajia kwenda nchini Morocco kuweka kambi ya maandalizi kuelekea msimu ujao wa mashindano.
 
Klabu ya RS Berkane ya Morocco inayofudishwa na Kocha Florent Ibenge imetuma ofa kwa klabu ya Yanga kwa ajili ya kumsajili winga Tuisila Kisinda.

Tayari nyota huyo ambaye yupo mapumziko nchini kwao DR Congo amepata VIZA ya mwezi mmoja (August 06 -September 06) kwenda nchini Morocco kukamilisha usajili huo.
 
Sadio Kanoute "fundi"
SIMBA SC
.
Kiungo wa timu ya Taifa ya Mali
na klabu ya Al Ahly Bengazi ya Libya, Sadio Kanoute yuko mbioni kutua Simba SC ili kuja kuongeza nguvu katika eneo la kiungo.
.
Kanoute ana mkataba wa miaka mitatu na Al Ahly Bengazi hivyo Simba watalazimika kuvunja mkataba wake.
 
ABDI BANDA
SIMBA, YANGA, AZAM

.
Aliyekuwa beki wa Highland Park na Baroka za Afrika Kusini, Abdi Banda anahusishwa huenda msimu ujao akacheza Ligi Kuu Bara.
.
Zipo tetesi amefikia makubaliano na moja ya vigogo wa soka la nchini, watu wake wa karibu wamethibitisha hilo.
 
Rekodi Simba balaa Yanga
.
Kipigo cha mabao 3-1 ilichopewa Yanga na Express ya Uganda juzi kwenye mechi ya mwisho ya Kundi A, imeifanya Yanga kuendelea kuteseka kuifikia rekodi ya Simba katika michuano ya Kombe la Kagame.
.
Yanga iliyotwaa taji la michuano hiyo mara TANO, imeng’olewa na kushindwa kutimiza ndoto za kuifikia idadi ya mataji waliyotwaa watani wao, Simba iliyo kinara kwa kulibeba mara SITA tangu 1974.
.
Jangwani walionekana wana nafasi kubwa baada ya Simba kujitoa kushiriki na kusalia kama moja ya timu iliyobeba mara nyingi taji hilo, lakini kutumia kikosi cha vijana na wale wasio na nafasi kikosi cha kwanza pamoja na wale wapya iliyowasajili iliwafanya watoke michuanoni wakiwa na alama mbili.
 
Jangwani inogile, Sasa ni zamu ya Bangala
.
Yanga wamerudi nchini DR Congo na sasa wanataka tena kuchukua beki mwingine na matajiri wa GSM wako katika hatua za mwisho kabisa kumleta beki Yannick Bangala Litombo.
.
Yanga imeshamalizana kila kitu katika makubaliano na Bangala ambaye wakati wowote wiki hii atawasili nchini kuja kusaini mkataba na klabu hiyo kongwe.
.
Bangala sasa anakuja kuchukua nafasi ya Mghana na aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Lamine Moro ambaye amesitishiwa mkataba baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…