Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,869
Watu zaidi ya 20 wakiwemo Watumishi watatu wa Wizara ya Ardhi wamenusurika kifo baada ya kushambuliwa na Wafanyakazi wa Wavamizi wa shamba la aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Marehemu Daudi Balali ambapo shambulio hili lilitokea wakati wakiendelea na zoezi la upimaji wa shamba hilo ambalo kwa sasa linamilikiwa na Familia ya Balali katika Kijiji cha Melela, Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero.
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Morogoro Frank Minzikuntwe amesema vurugu hizo zimetokea baada ya maamuzi ya Serikali ya kulipima eneo hilo ili liweze kupangwa upya baada ya kutelekezwa kwa muda mrefu huku Wananchi wanaolizunguka wakikosa maeneo ya kilimo.
Kamishna huyo amesema hali za Watumishi pamoja na Wananchi wengine zinaendelea vizuri baada ya kufikishwa katika vituo vya kutolea huduma za afya katika halmashauri hiyo.
“Dereva aliokolewa na Bodaboda wa pale Kijijini huku nyuma wale Watu (Wafanyakazi wa Wavamizi) wakachoma gari, pikipiki tatu, vifaa vya upimaji, laptop tatu zilizokuwa kwenye gari na mali nyingine, Wataalamu kwa kushirikiana na Wajumbe na Mgambo walikimbia kutoka eneo la shamba na kujiokoa.