Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210807-082802_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20210807-082830_Opera%20Mini.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoani Lindi limethibitisha kuwaua Watu wanne kati ya sita wanaoaminika kuwa ni Majambazi, hii ilikua ni kwenye majibizano ya risasi kati ya Watu hao na Polisi katika eneo la Nanganga Station.

Inaelezwa kwamba Watu hawa walikua wakielekea Wilaya ya Ruangwa baada ya kufanya matukio ya ujambazi katika Wilaya za Liwale na Nachingwea Mkoani Lindi na kupora fedha, vocha na simu za Wafanyabiashara zenye thamani ya shilingi milioni tano na laki mbili.
Screenshot_20210807-120722_GBInsta.jpg
 
Wengi wetu inawezekana tukiulizwa faida za miti kwenye Miji tunaweza kujibu labda ni kivuli tu na kupumzika chini yake ambako huwa na hewa nzuri ila Wataalamu wanasema kwenye utafiti wao kwamba ni jambo la muhimu sana kuwa na Miti kwenye mazingira ya nyumbani na hata kwenye Miji mbalimbali kwani kuna faida zaidi ya hizo nilizozitaja hapo juu.

Wataalamu wanasema miti pia ina uwezo wa kupunguza makali ya joto kwasababu inanyonya mionzi ya jua na kutoa maji hewani kupitia majani yake ambapo kwa kawaida sehemu za mijini huwa na joto kali sana wakati wa kiangazi........ utafiti uliowahi kufanywa Marekani umeonyesha kwamba miti inapofunika asilimia 40 ya Mji wowote inaweza kusaidia kupunguza joto kwa nyuzi joto 5 wakati wa kiangazi.
Screenshot_20210807-135850_GBInsta.jpg
 
Watoto hawa kwenye picha ya kwanza na ya pili wa kiume na wa kike ni miongoni mwa Washindi wa ASAS Half Marathon 2021 iliyofanyika leo Iringa.

Naibu Waziri wa Michezo Pauline Gekul Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga Mkuu wa Wilaya ya Iringa Moddy Moyo leo waliwaongoza Watanzania kutoka sehemu mbalimbali kushiriki kwenye ASAS Half Marathon.

Baadhi ya Washindi walipata zawadi ya Ng’ombe kutoka kwenye shamba la kampuni ya bidhaa za maziwa yenye makao yake makuu Iringa ya asas dairies maziwa pamoja na zawadi nyingine.
Screenshot_20210807-140030_GBInsta.jpg
Screenshot_20210807-140117_GBInsta.jpg
 
KARIA MINNE TENA

Wapiga kura 80 wamempitisha Wallace Karia kuongoza kwa mara nyingine Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwenye uchaguzi mkuu unaoendelea jijini Tanga.

Karia ameidhinishwa na wapiga kura baada ya kukosa mpinzani.
Screenshot_20210807-140456_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa idara elimu msingi halmashauri ya Jiji la Arusha, Omary Kwesiga amesema ameshangazwa kusimamishwa kazi akidaiwa kufanya igizo la kuchomwa chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 .

Amesema picha za video zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikionyesha kuwa hakuchomwa chanjo hiyo zimechezewa, na kubainisha kuwa alichanjwa.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Agosti 6, 2021 Kwesiga amesema anashangazwa na video hiyo, "nimezuiwa kuongea na vyombo vya habari kulingana na maadili ya kazi na kikubwa mimi nimechanjwa nina ushahidi na nipo Salama."
Screenshot_20210807-140707_GBInsta.jpg
 
Saikolojia inasema kumpongeza ( compliment) mtu kunafanya awe katika hali nzuri ( mtu anajisikia vizuri ) na wewe pia unayemsifu unakua katika mood nzuri.

Kwa mfano: unamwambia mtu daah! Nimependa style yako ya nywele au ukimsifu mtu kwa kusema hotuba yako ya leo ilikua nzuri sana basi wewe unakua ume-boost mood yako na yake pia wote mnakua mnajihisi vizuri.

Mimi naongezea isiwe ya kinafiki
Screenshot_20210807-150936_Instagram%20Lite.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom