Makapuku Forum

Rais Samia Suluhu Hassan, leo July 11, 2021 ametoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo kufuatia hasara kubwa waliyoipata kutokana na kuungua moto kwa Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar es Salaam.

Kufuatia hasara kubwa iliyotokana na kuungua kwa Soko hilo usiku wa July 10, 2021, Rais Samia ameviagiza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanya uchunguzi wa kina kujua chanzo cha moto huo.

Amesema Soko Kuu la Kariakoo ni soko kubwa Jijini Dar es salaam ambalo lina mkusanyiko mkubwa wa wafanyabiashara na kuteketea kwa soko hilo kutakuwa kumesababisha hasara kubwa kwa Wapangaji na Wamiliki wa soko hilo kongwe nchini.

Rais Samia amesema Soko la Kariakoo licha ya kuajiri Wafanyabiashara wengi lakini ni kitovu cha biashara kwa Nchi za Afrika Mashariki hivyo tukio hilo si hasara kwa Wafanyabiashara tu bali hata kwa Serikali.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wafanyabiashara katika soko la Kariakoo wawe watulivu wakati Serikali inafanya kazi yake ya kujua chanzo cha moto huo na amewahakikishia usalama wa mali zilizo ndani ya soko hilo

Waziri Mkuu pia amewataka Wafanyabiashara kutoingia ndani ya soko hilo katika kipindi hiki ambacho udhibiti unaendelea hadi pale timu zilizoundwa zitakapojiridhisha na utulivu na kufanya sensa ya Watu wenye mali kuingia mmoja baada ya mwingine ili wakatoe vitu walivyoviacha.

“Tunachoshukuru kule chini shimoni hakuna moto, mali zote zinalindwa, msiwe na mashaka milango yote imefungwa na Makamanda wako ndani na nje wanalinda, mali zote zimehifadhiwa, msiwe na mashaka”———-Majaliwa
 
Fire zote kubwa kubwa za private, zimeshindwa kwenda kuuzima moto...

Za serikali tunajuaga mambo yao, hawanaga maji kila siku...

Inasikitisha sana...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…