Makapuku Forum

Makapuku Forum

Volkswagen na Porsche zimeingia makubaliano na kampuni maarufu ya kutengeneza magari ya Croatia iitwayo Rimac ili kuanza kutengeneza gari aina ya Bugatti linalotumia umeme.

Pamoja na kufunguliwa kwa Kampuni hiyo mpya ya Bugatti-Rimac, Bugatti itaendelea kama kawaida kutengeneza magari yake ya mafuta nyumbani kwa kampuni hiyo Moisheim, Ufaransa.

Kampuni inayotengeneza magari ya Bugatti ilianzishwa mwaka 1909 na kupata soko la kuuza magari hayo kwa Matajiri na Watu maarufu.
20210706_042145.jpg
 
Mchezaji wa Minnesota FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS) Hassani Dotson hakutaka kutoka uwanjani kabla ya kumvisha pete ya uchumba Mpenzi wake Petra Vuckovic baada ya mechi ambapo alifanya tukio hilo baada ya sare ya 2-2 vs San Jose Earthquake.
20210706_042331.jpg
20210706_042400.jpg
20210706_042415.jpg
 
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kutangaza mipango ya kuondoa sheria inayowalazimu Watu kuvaa barakoa na hatua ya kuweka umbali kati ya Mtu na Mtu na sasa Waziri huyu Mkuu anasema ataelezea jinsi Nchi hiyo itakavyojifunza kuishi na virusi hivyo.

Kabla ya kukutana na Waandishi wa Habari, Waziri Mkuu Johnson aliashiria kuwa sheria za lazima zitabadilishwa baada ya July 19 siku inayotajwa na Vyombo vya habari vinavyoegemea mrengo mkali wa kulia kuwa ni siku ya ''Uhuru''.

Vizuizi hivyo vitaondolewa katika kipindi cha wiki mbili zijazo licha ya kiwango cha maambukizi ya virusi hivyo kuongezeka kutokana na kusambaa kwa aina mpya ya kirusi cha corona kiitwacho Delta, mpango huu wa Johnson ni ni tafauti kabisa na mtazamo aliokuwa nao mwanzoni wakati corona ikianza kuitepetesha Uingereza.
20210706_042525.jpg
 
Umoja wa Mataifa umetabiri kwamba ulaji wa nyama nyekundu katika Nchi zilizoendelea kiviwanda utapungua katika kipindi cha miaka 10 ijayo, ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na chakula na kilimo FAO iliyotolewa leo huko Rome, Italia imeeleza kwamba hatua hiyo inatokana na kuongezeka wasiwasi wa kimazingira na kiafya.

Ripoti hiyo imesema Watu watapunguza ulaji wa nyama na hasa nyama nyekundu na kugeukia zaidi nyama ya ndege kama kuku au bidhaa za maziwa, hii ni Ripoti ya leo ambayo imehusisha Shirika la FAO na shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo OECD ambapo Watalamu wametoa mtazamo wao kuhusu hali ya kilimo duniani hadi mwaka 2030.
20210706_042658.jpg
 
Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta amekamilisha uhamisho wake wa kudumu kuitumikia Club ya Fenerbahce ya Uturuki akitokea Aston Villa ya England.

Samatta awali alijiunga na Fenerbahce kwa mkopo akitokea Aston Villa baada ya kukaa kwa miezi sita na nafasi yake ikazibwa na Watkins.

Mwisho wa msimu wa 2020/2021 Samatta alipaswa kurejea Aston Villa ila ameamua kusaini mkataba wa kudumu baada ya Aston na Fenerbahce kuafikiana, Samatta alijiunga na Aston Villa January 2020 akitokea KRC Genk ya Ubelgiji.
20210706_042808.jpg
 
Watoto wawili Manyirizu Joseph mwenye umri wa miaka sita na Bertha Mateso mwenye miaka mitano wamefariki na wengine kunusurika baada ya kula kiporo cha wali na nyama ya kondoo kutoka kwenye sherehe ya mahari iliyofanyika Ikobe, Mbogwe Mkoa wa Geita.

RPC Henry Mwaibambe ameiambia AMPLIFAYA ya CloudsFM ———> "Tarehe 30 June 2021 kulikua na sherehe nyumbani kwa Kasongwe, Watu walikula na kutawanyika bila madhara yoyote lakini kesho yake asubuhi Wageni na Wenyeji waliokua wamebaki pale waliamkia kiporo"

"Baada ya kula walianza kuharisha na kutapika ambapo Watoto hawa ndio wakafariki huku Watoto wengine 15 wakilazwa Hospitali Watu wazima wakiwa watatu, hali zao zinaendelea vizuri, mpaka jana jioni 13 walikua wameruhusiwa, tumechukua sampuli za chakula kufanya upelelezi kujua kilichopelekea tatizo hili" ——— RPC Mwaibambe.
20210706_043136.jpg
 
Kutoka kwenye ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Mwl.Nyerere (JNHPP) kwenye Bonde la Mto Rufiji leo July 5, 2021 ambapo Marais Wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete na Mawaziri Wakuu Wastaafu Cleopa Msuya, John Malecela na Mizengo Pinda wametembelea mradi huu mkubwa wa kuzalisha umeme.

Mradi huu unatarajiwa kukamilika June, 2022 na utazalisha umeme Megawati 2115 ambazo zikijumlishwa na megawati 1,500 zinazozalishwa na vyanzo mbalimbali nchini hivi sasa zitaifanya Tanzania kuwa na umeme utakaotosheleza mahitaji yake na ziada kuuzwa kwa Majirani.
20210706_043445.jpg
20210706_043607.jpg
20210706_043622.jpg
20210706_043800.jpg
 
Kiongozi wa kiroho wa Wakatoliki na Rais wa Vatican, Papa Francis ambaye amelazwa Hospitali kwa upasuaji kutokana na shida katika utumbo wake mkubwa anaendelea vizuri baada ya upasuaji lakini atalazimika kubaki Hospitali kwa siku saba akiwa chini ya uangalizi wa Madaktari.

Taarifa kutoka Vatican inasema Papa alipelekwa katika Hospitali ya Gemelli huko Roma jana Jumapili alasiri kwa upasuaji wa dalili ya ugonjwa wa 'colon diverticulum stenosis'.
20210706_043931.jpg
 
Idadi ya waliofariki kwenye ajali ya ndege ya kijeshi ya Ufilipino aina ya C-130 imeongezeka na kufikia 50 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo.

Ndege iliyokuwa imebeba jumla ya Wanajeshi 96 ilianguka jana jumapili katika mji wa Patikul ulioko kwenye kisiwa cha Jolo kiasi kilomita 1000 kutoka mji mkuu Manila.

Wizara ya ulinzi jana ilisema Wanajeshi 47 walifariki na raia wanne waliojeruhiwa wako hospitali.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa ndege hiyo ilizingatia utaratibu wa kuelekea kutua na hali ya hewa pia ilikuwa nzuri wakati wa kutuwa lakini iliacha barabara na baadae kulipuka.
20210706_044242.jpg
20210706_044259.jpg
 
Moto ambao chanzo chake hakijajulikana umeteketeza moja ya chumba cha darasa katika shule kongwe ya sekondari Geita.

Chumba hicho kilikua kimehifadhiwa magodoro pamoja na masanduku ya vyuma ya wanafunzi.

Wanafunzi wengi wameripoti shule Leo Jumatatu Julai 5, 2021 kwa ajili ya kuanza masomo.

Katika tukio hilo hakuna aliyejeruhiwa.
20210706_045108.jpg
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo leo Julai 5, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na wazee pamoja na waasisi wa chama hicho katika ofisi kuu ya CCM Zanzibar, Kisiwandui.

Akizungumza na wazee hao, Chongolo ametoa salamu za shukrani kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan za kuwashukuru wazee kwa kuendelea kusimamia maadili katika jamii na kuwa mstari wa mbele kutoa ushauri mbalimbali ndani ya chama na Serikali.
20210706_045227.jpg
 
Ameandika msemaji wa Simba, Haji Manara kuelekea mechi ya fainali kombe la Azam Shirikisho Julai 25 mkoani Kigoma.

"Unafika Pemba kutokea Airport hadi kinyasini Wete Pemba kote barabarani watu wametinga jezi za Mnyama.

Wapemba hawajali kuhusu matokeo ya juzi,,before sikuwa najua Pemba ina Simba wengi kiasi hiki aiseee.

Captain john Bocco sema na wenzio bro,,,mtakuja kuua watu Kwa makundi siku moja ,naambiwa Dar kuna Shabiki kajipiga kitanzi huko,,,half ya kwanza mmecheza kama mmelazimishwa au mnadai kitu,,mmezinduka second half na wao wakaweka contena mechi ikaisha,,,,

Wallah kigoma tukifungwa naacha hii kazi narudi Shamba kulima,,,,viongozi wanatimiza majukumu yao,Washabiki wanajaa kuliko Washabiki wao kwa mbali mno,,mm natukanwa kutwa Kwa kuwapa nguvu nyie lakini mmeenda kutuangusha,,,,

Sioni sababu ya kuendelea na kazi hii kama wachezaji hawajui nn maana ya uzito wa Derby,,,Wachezaji wao wanajitoa asilimia elfu moja toka dakika ya kwanza,,,cc tunazinduka kushakuchwa,,,,kaeni wenyew zungumzeni na thamani ya jezi ya simba ilindwe"
20210706_045338.jpg
 
Polisi katika Wilaya ya Rakai nchini Uganda wanachunguza mazingira ya tukio ambalo nguruwe anasemekana kuua mtoto wa mwezi mmoja aliyekuwa ndani ya nyumba ya mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Kateera katika Kaunti ndogo ya Ddwaniro, Wilaya ya Rakai baada ya mama wa mtoto huyo, Peace Tukwasibwe kumuacha mtoto ndani ya nyumba na kwenda shamba kutafuta kitafunwa kwa ajili ya kifungua kinywa.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya mama huyo kurudi alikuta sehemu chache za mwili za mtoto zilizobaki huku nguruwe akiwa amelala kwenye godoro ambalo mtoto alikuwa amelalia.
20210706_045642.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom