Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210628_064011.jpg
20210628_064028.jpg
 
Mwimbaji wa Nigeria Burnaboy ameshinda Tuzo ya Msanii bora wa kimataifa kwenye Tuzo za BET 2021 zinazoendelea kutolewa muda huu Los Angeles Marekani.

Tuzo hiyo ilikua ikiwaniwa na Wakali mbalimbali akiwemo Mtanzania Diamond Platnumz, Wizkid na Mwimbaji wa Ufaransa/Mali Aya Nakamura.
20210628_065611.jpg
 
UNAAMBIWA

Ibrahim Yucel kutoka Uturuki ameamua kubuni kitu kinachofanana na Helmet na kuvaa kichwani huku kikiwa kinafungwa na kufuli wakati wote hadi pale anapotaka kula kwa lengo la kumsaidia kuacha sigara, kifaa hicho ambacho kinafanana pia na zizi la ndege kinafungwa na funguo anatembea nazo Mkewe.

Uamuzi huo umekuja baada ya Ibrah kubaini kuwa amekuwa akivuta pakiti mbili za sigara kwa siku tangu akiwa na umri wa miaka 16 lakini Baba yake alipofariki kwa Kansa ya Mapafu akaona ni vizuri aache kwa faida yake ya kiafya yake na apate muda wa kujitunza Familia kwa kuepuka matumizi makubwa ya pesa kwenye sigara.
20210628_165632.jpg
 
“Nilishasema nitakaa na wenzangu Wanasiasa tuone tunakwenda na siasa zetu katika mustakabali mpana wa Taifa, Nchi yetu ina vitu vingi, Corona inatupiga, uchumi umeshuka tunaupandisha nimesema nakwenda kuifungua Nchi naomba nipeni muda halafu tutakwenda kwenye mengine”——Rais Samia akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari Dar es salaam leo

“Mnasema nimeanza vizuri naomba nipeni muda nisimamishe Nchi kiuchumi, tuite Wawekezaji uchumi upande, halafu tutazungumzia mengine, tutazungumzia Katiba Mpya, mikutano ya hadhara n.k, kwa sasa mikutano ipo ya ndani na Wabunge kwenye Majimbo yao pia wanafanya”———Rais Samia
20210628_180849.jpg
 
“Kuhusu Corona maamuzi yetu ni kwamba twende na Dunia inavyokwenda, niwe mkweli Tanzania tuna Wagonjwa wa Corona, kwa takwimu nilizonazo tuna Wagonjwa kama 100 na kitu, na kati yao Wagonjwa 70 naa, wapo kwenye mitungi na wengine matibabu ya kawaida”———Rais Samia akizungumza na Wahariri wa Vyombo Vya Habari Dar es salaam leo
20210628_181053.jpg
 
“Tumeamua tuchanje (ili kujikinga na Corona) na tumeamua tuchanje kwa hiari, anayetaka atachanja na asiyetaka asichanje na wapo Watanzania wengi wakiwemo Wafanyabiashara ambao wamechanja wengine Dubai na maeneo mengine (nje ya Nchi)”———Rais Samia Suluhu akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari Dar es salaam leo

“Tumeamua pia Jamii ya Kimataifa ichanje na tutawasimamia, kwa upande wetu kuna Mpango wa COVAX, June 15 ndio mwisho kwa watakaopata chanjo 2022 na sisi tumeharakisha kusema na sisi tumo, hivyo Wataalamu wetu wanakaa kuangalia ni kivipi?”———Rais Samia

“Mpaka sasa yameshajitokeza Mashirika mengi yanataka kutusaidia, ila tunasubiri Wataalamu waseme ni chanjo ipi tuchanje, kwahiyo hilo tunalifanyia kazi”———Rais Samia
20210628_181216.jpg
 
“Kuhusu magazeti yaliyofungiwa Waziri amesikia, lakini kuna magazeti yamemaliza leseni wakaanze mchakato wapewe leseni waendelee, niseme tu hapa kwamba sheria za Nchi lazima zifuatwe kuna zile adabu na heshima za kiafrika zizingatiwe”

“Kuhusu hili la leseni za vyombo vya habari kulipwa kwa Dola hata nami naliona kuwa ni changamoto, hatuwezi kuwa Watumwa wa Sheria tunazozitunga, tutakaa kitako tuangalie tunakwendaje”

“Huwezi kukaa tu na gazeti lako ukamchambua tu Mama Samia mengine ya kweli na ya uongo as if kwenu hauna Mama sio adabu na heshima ya Kiafrika mkifanya hivyo hakuna atakayefungiwa, tukosoane ila pia tupeane njia ya kufanya, sikatai tukikosea tutaomba radhi tutasonga”———Rais Samia akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari Dar es salaam leo
20210628_183023.jpg
 
“Kuhusu Vyombo vya Habari kufungwa kwa kuyumba kiuchumi kwasababu ya kunyimwa matangazo sijalikuta kwenye meza katika faili zote nilizoletewa hili sikulikuta, kama kulikuwa na katazo sikulikuta ila nawahakikishia katika wakati wangu huu sitokataza”

“Niwape mfano kule Zanzibar Network yote ya Suluhu tumefungua TV, Suluhu TV lakini hatujapata matangazo mpaka leo tunachanga tunalipa mishahara ya Wahariri na wengine, wito wangu changamkieni matangazo”

“Nina ombi la kuangalia chombo cha Msemaji Mkuu wa Serikali kuifanya Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kusimama yenyewe, tutaangalia na haya mengine na hatutofanya pekee yetu tutawaita Wahariri na Watu wa Vyombo vya Habari tuangalie tunafanyaje”

“Kuna suala la kwanini Baraza lisipate ruzuku ya Serikali kama Bunge na Mahakama, hapa Sheria inanibana hii ni Mihimili ya Serikali na ni lazima ipate ruzuku, Jukwaa bado halijawa ila tuendeleee na mazungumzo tuone tunafikia wapi”———Rais Samia kwenye Mkutano wake na Wahariri wa Vyombo vya Habari
20210628_190219.jpg
 
“Niwaambieni bila kupepesa macho kazi ya Urais ni ngumu lakini kwasababu Urais ni Taasisi yenye vyombo kadhaa vinavyosaidia ndipo urahisi wake ulipo, Rais hafanyi kazi pekee yake”

“Nikisikia Watu kwa kundi kubwa mnasimama mnasema Mama kafanya mazuri, inanipa moyo ndio maana tunazungumza na makundi, Watanzania ni Watu wa moyo ukiwafanyia kidogo wanashukuru, maombi kila pembe Misikitini na Makanisani, shukrani inanipa moyo”

“Tuchukue tahadhari dhidi ya Corona ukihisi nyungu inakusaidia fanya, ukihisi dawa gani sijui yakusaidia tumia, ila sisi tunasisitiza zile ambazo Wataalamu wanatuambia kunawa mikono kwa maji tiririka, kutumia barakoa n.k”

“Tiba asili zimetibu generation to generation na ndio maana Serikali imeweka Bodi, Wataalamu wakae watazame zile wanazoona zinakidhi vigezo zitumike, kuna wakati tunabeza lakini zinasaidia, hatuwezi kubeza moja kwa moja, Wanasayansi tu watusaidie”

“Kuhusu kuihamishia Idara ya Habari kwenye Wizara ya Teknolojia ya Habari tutakaa tuangalie kwa pamoja tukijiridhisha vya kutosha tunaweza kuangalia vinginevyo”———Rais Samia akizungumza na Wahariri Dar es salaam leo.
20210628_190403.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom