Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 25,012
- 56,303
Ilikuwa siku kama ya leo, anyway Mussolin5 ulipotelea wapi?1986 - Kombe la Dunia mwaka 1986 nchini Mexico: Mechi ya robo fainali baina ya Uingereza dhidi ya Argentina inafanyika.
Diego Maradona, nahodha wa Argentina anafunga magoli mawili murua na kuitoa England kwa jumla ya magoli 2-1.
Goli la kwanza, Maradona alilifinga kwa mkono na goli hilo linajulikana kama Goli la Mkono wa Mungu.
Goli la pili, Maradona alipiga chenga wachezaji watano wa England kabla ya kufunga. Goli hili linajulikana kama Goli la Karne.
Hiyo ni moja kati ya mechi za kukumbukwa za wakati wote katika historia ya mchezo wa soka.
umenikumbushaa hii kituIlikuwa siku kama ya leo, anyway Mussolin5 ulipotelea wapi?
Nilishaweka we mzeeHahahaha nasubiri magazeti
Mzima kipenzi
Pole yao sana wafiwa...Idadi ya vifo kutokana na ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo ikihusisha magari matatu ambayo ni Toyota Coaster, Toyota Cresta na Lori eneo la nanenane mkoani Morogoro imeongezeka na kufikia Watu 9 kutoka Watu watano jana usiku.
Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dr. Kesy Ngalawa amesema pia majeruhi watano wa ajali hiyo wapo Chumba maalum cha Uangalizi (ICU).
Mmoja wa majeruhi Frank Ramsoni amesema Toyota Coaster ilikua inatoka Dar kwenda Mbeya na Dereva aliweka mashada kwenye gari hilo kuashiria imebeba maiti ili kupata wepesi wa kufanya safari ambapo baada ya kufika eneo la Kingulwira Morogoro gari lilisimamishwa na Askari.
Dereva wa gari alishuka kisha Msaidizi wake alichukua gari na kuondoka bila ruhusa ya Askari na wakati yuko barabarani gari likiwa kasi Msaidizi alimpigia simu mwenzake aliebaki na Askari na hapo ndipo akashindwa kulimudu gari likapoteza mwelekeo na kugongana uso kwa uso na lori la Kampuni ya Dangote.
R.I.PView attachment 1826701View attachment 1826702View attachment 1826703
Mbona mkuu wa wailaya mpya wa TMK kanuna hivyo...Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu mpya wa Wilaya hiyo ya Temeke Jokate Mwegelo. View attachment 1826709View attachment 1826710
Danganya toto ndiyo ishatoka hivyo...Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba amesema mfumo wa ulipaji wa kodi ya majengo kwa kutumia mita za Luku haitawahusu wapangaji bali ni wamiliki wa nyumba husika.
Ametoa mfano wa ilivyokuwa kwamba mpangaji anapokuwa amelipa malipo yoyote yaliyopaswa kufanywa na mmiliki huwa anawasiliana na mwenye nyumba wake ili arudishiwe hela yake.
Amesema mambo mengine yote yatapangiliwa vizuri ili kuepusha Watu kupanga foleni ya kwenda kulipa kodi ya pango.
Katika hatua nyingine Bunge limepitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 ambapo Wabunge 361 sawa na asilimia 94 wamekubali na Wabunge 23 sawa na asilimia 6 hawakuamua kwa kutokuwa na upande wowote.View attachment 1826692