Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amemuapisha Basilla Mwanukuzi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Basilla aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998.
Mkuu wa Wilaya Rorya Juma Chikoka maarufu Chopa Mchopanga ametembelea na kukagua mazingira ya Shule ya Msingi Utegi iliyopo Wilayani humo, muda mfupi baada ya kuapishwa hii leo.
Akiwa Shuleni hapo pamoja na mambo mengine DC Chikoka amewaagiza Walimu kuhakikisha wanasimamia na kutunza vizuri miti ya asili iliyopo Shuleni hapo kwa lengo la kudumisha utunzaji wa mazingira.
Kutoka katika ukumbi wa Anatoglo Mnazi Mmoja, hizi ni picha za matukio mbalimbali yaliyojiri wakati wa RC wa Dar es salaam Amos Makalla akiwaapisha Wakuu wapya wa Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Dar es salaam mapema leo.