Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amemuapisha Nickson Simon maarufu nikki wa pili kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe akichukua nafasi ya Jokate Mwegelo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, zoezi la kuapishwa limefanyika kwenye Ofisi ya RC Pwani iliyopo Kibaha.
Wasanii wanaounda kundi la HipHop la Weusi akiwemo Joh Makini, Lord Eyes na G Nako ni miongoni mwa waliofika kwenye Ofisi ya RC Pwani iliyopo hapa Kibaha kushuhudia zoezi la uapisho wa Ma-DC wa Wilaya zilizopo Mkoani Pwani akiwemo Msanii mwenzao wa Weusi Nickson Simon maarufu ambaye ameapishwa na RC wa Pwani Abubakari Kunenge leo kuwa DC wa Kisarawe.