Alizaliwa kama Temitope Balogun Joshua mnamo tarehe 12 mwezi Juni katika jimbo la Ondo nchini Nigeria.
Kulingana na Mtandao wa kanisa lake la SCOAN , Joshua alikuwa ndani ya tumbo la mamake kwa miezi 15 kabla ya kuzaliwa kwake.
Akiwa shuleni alijulikana kama muhubiri mdogo kutokana na alivyokuwa akiipenda Biblia na uwezo wake wa kutabiri matukio yaliofanyika katika jamii yake , kwa mujibu wa mtandao wa SCOAN.
Alianzisha kanisa la SCOAN mwaka 1987 akiwa na waumini wachache kabla ya kanisa hilo kupanuka hadi kimataifa.
Mwaka 2009 TB Joshua alianzisha klabu ya kandanda kwa jina My people FC katika juhudi za kuwasaidia vijana.
Kulingana na jarida la Forbes 2011 , Temitope Joshua ni muhubiri wa tatu tajiri nchini Nigeria akiwa na thamani ya $15m.
TB Joshua ana makanisa mengi katika mataifa tofauti barani Afrika na Marekani ya kusini.
Mungu amechukua maisha ya muhudumu wake TB Joshua. Amefariki akimtumikia Mungu, imeandika taarifa rasmi kutoka SCOAN na kuongeza kuwa maneno ya mwisho ya TB Joshua alisema
“Watch and Pray” “One life for Christ is all we have”.