Makapuku Forum

Mbunge Esther Matiko
Mh na huyu yumo?
 
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amewasili leo mjini Cairo wakati akiendeleza juhudi za kuuongeza nguvu mpango wa kusitisha mapigano uliofikiwa kati ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza. Akiwa Cairo, Blinken atakutana na Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi kabla ya kuelekea Jordan kwa mazungumzo na Mfalme Abdullah II.

Baada ya mazungumzo na rais wa Wapalestina Mahoumd Abbas katika makao yake makuu ya Ukingo wa Magharibi hapo jana, Blinken aliapa kuyajenga upya mahusiano ya Marekani na Wapalestina kwa kufungua upya ubalozi mdogo mjini Jerusalem pamoja na kuwapa msaada wa mamilioni ya dola kwa ajili ya ujenzi wa Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita.

Alikutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kusisitiza uungwaji mkono wa Israel kujilinda yenyewe dhidi ya mashambulizi ya maroketi kutoka kwa wanamgambo wa Hamas.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…