Makapuku Forum

Makapuku Forum

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema hadi sasa Magazeti ambayo yamefungiwa kisheria Nchini Tanzania ni manne ambayo ni Mawio, Mseto, Mwanahalisi na Tanzania Daima ambapo hatua kadhaa zinaendelea ndani ya Serikali ili kuyafungulia magazeti hayo.

“Ninachofurahi ni kwamba hadi leo hii hakuna Redio hata moja au TV iliyofungiwa isipokua Online TV moja, Radio ni moja ilikua Wasafi FM wakati fulani lakini tukawaambia wafanye mapitio na sasa inaendelea na kazi, Magazeti manne yaliyofungiwa hatua zinaendelea ili warejee kwenye uandishi wao, kwa kuwa yalifungiwa kwa mujibu wa sheria basi sheria zilezile zitafata utaratibu wake kwa maelekezo ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, hiyo ndio nia nzuri, nia njema ya Serikali yetu"

"Kwa miongozo ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan hatudhani kama kutakua na jambo gumu lakini pia ni muhimu nasi tukaendelea kuheshimu kanuni, taratibu na sheria tulizonazo katika kufanya kazi yetu" - Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo akiongea na Jukwaa la Wahariri.
20210520_190430.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amekanusha taarifa za yeye kuzindua kiwanda cha kutengeneza sehemu za siri za mfano.

“Nimeona article ya uongo ikisambaa kwenye mtandao ikionyesha nazindua kiwanda cha kutengeneza sehemu za Siri za mfano “dildo” za mwanaume, napenda kukanusha habari hizi sio za kweli”

“Hiyo picha ilichukuliwa katika mafunzo ya kupambana na UKIMWI miaka minne iliyopita Chuo Kikuu Mkwawa, Msambazaji alikuwa na nia ovu tu juu yangu, nimemwagiza Mwanasheria wangu analifanyia kazi jambo hili” ———
20210520_190624.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amekanusha taarifa za yeye kuzindua kiwanda cha kutengeneza sehemu za siri za mfano.

“Nimeona article ya uongo ikisambaa kwenye mtandao ikionyesha nazindua kiwanda cha kutengeneza sehemu za Siri za mfano “dildo” za mwanaume, napenda kukanusha habari hizi sio za kweli”

“Hiyo picha ilichukuliwa katika mafunzo ya kupambana na UKIMWI miaka minne iliyopita Chuo Kikuu Mkwawa, Msambazaji alikuwa na nia ovu tu juu yangu, nimemwagiza Mwanasheria wangu analifanyia kazi jambo hili” ——— View attachment 1791963
Mzee wa kutuliza.
 
Leo May 21, 2021 Kwenye Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 3, Air Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk. Leonard Chamuriho pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Mhandisi Matindi wamezindua ukumbi wa kupumzikia abiria unaoitwa Twiga Business Lounge uliopo Terminal 3 ambao una uwezo wa kuhudumia Watu 200 kwa wakati mmoja.
20210521_155129.jpg
20210521_155153.jpg
20210521_155217.jpg
20210521_155255.jpg
 
Ni taharuki kwenye eneo la Nordend mji mkubwa wa kibiashara wa Ujerumani baada ya kugundulika bomu lenye takribani kilo 500 ambalo ni la vita kuu ya pili ya dunia, taharuki hiyo imefanya wengi kuogopa na kuondolewa kwenye makazi yao kwa muda.
20210521_160653.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amemaliza sintofahamu ya uongozi wa Manispaa iliyojitokeza kati ya Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Spora Liana.

Utatuzi wa mgogoro huo umefanyika leo katika kikao cha pamoja kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa na kuwakutanisha Meya na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni.

Makalla amewataka Viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za Wananchi, Meya na Mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa maslahi mapana ya Wananchi.
20210521_160907.jpg
20210521_160927.jpg
20210521_160951.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom