Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210504_062900.jpg
20210504_062917.jpg
 
Mbunge wa Muheza Tanga ambae pia ni Msanii, Hamisi Mwinjuma MwanaFA amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu kanuni iliyoanza kutumika na BASATA ya kukagua nyimbo za Wasanii wote Tanzania kabla ya kupelekwa Redioni.

Kupitia XXL ya Clouds fm amesema ———> "Sidhani kama muziki unahitaji mipaka mingi kiasi hicho japokua siungi mkono kuwa na lugha chafu au maneno ya matusi kwenye nyimbo sababu muziki unasikika sana na tunaharibu hata Watoto mapema na kutengeneza matabaka flani nyimbo haziwezi kusikilizwa ukiwa na Mtu flani"

"Niliuliza hili swala kwenye group la Whatsapp wakasema wanataka kutumia software kufanya shughuli hii mimi nikauliza kama BASATA wanaweza kutumia software kufanya shughuli hii software haiwezi kujua mafumbo na Watu wakitumia mafumbo kwahiyo kama ni bora wasitumie kitu waziache nyimbo ambazo hazina matusi ya moja kwa moja zipigwe tu Redioni"

"Hii sheria ya kimsingi ya kupitisha nyimbo BASATA zikasikilizwe kwanza kabla ya kupelekwa Redioni sifikiri kama ina msingi wowote lakini sheria ni sheria acha tuiangalie huku tuongee na Watu wa Wizara, tuongee na Waziri, Katibu Mkuu kuona namna marekebisho yanaweza kuja ya sheria ili mradi iondoke na iache muziki huru, kimsingi mimi siko nayo na naamini haki itatendeka na haitoendelea kutumika kuwabana Wasanii na kuurudisha muziki nyuma" ———
20210504_164034.jpg
 
“Nashukuru sana Rais Kenyatta kwa makaribisho mazuri,tumeongea mengi ila kubwa ni uhusiano, nimemwambia Kenyatta kuwa Kenya inashika nafasi ya 5 Duniani kwa uwekezaji Tanzania, imewekeza miradi 513 yenye thamani ya USD Bil 1.7 ambayo imetoa ajira Elfu 51 za Watanzania”———Rais Samia akiwa Kenya

“Naahidi Tanzania sasa tutakuja kwa nguvu yote Kenya kuja kuwekeza ili kukuza ujazo wa kibiashara, tuna fursa kubwa katika Nchi zetu sasa tunakwenda kutumia fursa hizi kukuza biashara kati ya Tanzania na Kenya na katika Mataifa mengine”———Rais Samia

“Tumejadiliana pia kuhusu namna ya kupata nishati (umeme au gesi) kutoka upande mmoja kwenda mwingine, tuna hiyo miradi mmoja tulishasaini mkataba leo na Kuna mmoja mazungumzo yapo karibu kumalizika, nitumie lugha ya Rais Kenyatta tutaweka kidole hivi karibuni”———Rais Samia
20210504_164231.jpg
 
“Hii ni safari ya kihistoria na inadhihirisha uhusiano wetu (Kenya na Tanzania) tangu tukiwa tunapigania Uhuru wetu, ni Safari ya kwanza kutembelewa na Rais Mama wa kwanza katika Jumuiya yetu kwahiyo tunakupongeza na tunakupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM”———Rais Uhuru Kenyatta

“Tumefanya mazungumzo na Rais Samia na tumewaelekeza Viongozi walio chini yetu kuondoa kero ndogondogo zinazowasumbua Wafanyabiashara na Wewekazaji wa Nchi zetu wanapotoka Nchi moja kwenda Nchi nyingine”——- Kenyatta

“Tuko na furaha tele kukukaribisha Rais Samia kwasababu tunakuona kama Dada yetu, tutaendelea kudumisha uhusiano mwema, Undugu na uchumi mwema wa Wananchi wa Kenya na Tanzania na Afrika Mashariki”———Kenyatta
20210504_164344.jpg
 
Kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson leo ametembelea Lowry Hotel iiliyopo katika jiji la Manchester ilipofikia timu ya PSG ambapo usiku wa leo inacheza na Man City katika marudiano ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
20210504_164741.jpg
 
“Mwaka huu December 09, Tanzania tunatimiza miaka 60 ya Uhuru wetu na nimetoa mwaliko rasmi kwa Rais Kenyatta awe Mgeni rasmi katika Maadhimisho yale ya miaka 60 ya Uhuru wetu”———Rais Samia Suluhu mbele ya Rais Kenyatta ziarani Kenya leo
20210504_165508.jpg
 
Hivi ndivyo Rais Samia Suluhu Hassan alivyokagua gwaride akiwa Ikulu ya Kenya mbele ya Mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais Samia yupo Kenya kwa ziara rasmi ya siku mbili kwa mwaliko wa Kenyatta.
20210504_165635.jpg
 
Hivi ndivyo Rais Samia Suluhu Hassan alivyopigiwa mizinga ya heshima akiwa Ikulu ya Kenya mbele ya Mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais Samia yupo Kenya kwa ziara rasmi ya siku mbili kwa mwaliko wa Kenyatta.
20210504_165739.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom