Makapuku Forum

Makapuku Forum

“Binafsi huwa nashangazwa sana na wale ambao wanadhani kuwa eti Kenya na Tanzania ni washindani na kwamba uhusiano wetu unapaswa kuwa wa kukamiana na mbaya zaidi ni kule kuamini kwao kwamba hilo linawezekana tu mmoja wetu kumwangusha mwenzake”———Rais Samia Bungeni Kenya leo

“Watu (wanaoamini Tanzania na Kenya ni Washindani) ni wenye choyo, maono mafupi na akili mbovu, bahati mbaya Watu hawa wapo kwenye pande zote Kenya na Tanzania na wapo ambao wapo kwenye Serikali zetu na Wanasiasa, bahati nzuri sio wengi ndio maana uhusiano wetu unadumu”———Rais Samia

“Kwa yeyote anayefikiria kuleta uhasama baina yetu, ujumbe wangu kwao ni kwamba Tanzania na Kenya, tulikuwepo, tupo na tutaendelea kuwepo, iwe kiangazi iwe masika Tanzania na Kenya tutaendelea kuwepo”———Rais Samia

“Badala ya kunyang’anyana Watalii tuongeze vivutio vyetu vitakavyomfanya Mtalii aongeze siku za kukaa Kenya na Tanzania, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema; tukipoteza muda mwingi kugawana kibaba tutapoteza muda mzuri wa kuvuna kikubwa” ———Rais Samia
20210505_192842.jpg
 
“Tumekuwa na mazungumzo mazuri na yenye kuamsha matarajio makubwa sana kwa Nchi zetu mbili, kwa yale tuliyotofautiana hayakuwa na misingi ila tu ni mitazamo tofauti ya Watu, uchungu wowote uliojitokeza ulikuwa uchungu wa uzazi na sio wa maradhi”———Rais Samia Bungeni Kenya

“Uchungu wa uzazi unaishia kuleta Mtoto na unaleta furaha kwenye Familia lakini uchungu wa maradhi unaishia kwenye kifo, sisi (Tanzania na Kenya) tunapokerana huo ni uchungu wa uzazi, tukae tuzungumze tupate Mtoto Amani tuendelee na uhusiano wetu”———Rais Samia

“Chini ya uongozi wangu, tutafanya kila tunachoweza ili kuimarisha uhusiano wetu, Dira ya Serikali yangu ni kudumisha ya awamu iliyopita na kuendeleza mapya, kama kuna ambalo linalega au uhusiano wetu unasuasua nimekuja kuyanyoosha yale yaliyojipindapinda”———Rais Samia

“Kenya ndio Nchi ya kwanza kwa mimi kufanya ziara rasmi, nilienda Uganda kusaini mkataba ila haikuwa ziara rasmi, ziara yangu ya kwanza rasmi tangu kushika Uongozi nimeanzia Kenya na sio kwasababu ni karibu kijiografia ila ni kwasababu ya umuhimu wa Kenya kwa Tanzania”———Rais Samia
20210505_193307.jpg
 
“Corona imefanya tubadili mfumo wa maisha, hivi tunavyoishi tumevaa barakoa inanikumbusha Kijijini kwetu wakati tunapeleka mbuzi machungani tunawafunika kama hivi ili kuwazuia wasile mazao ya Watu, leo wanadamu ndio tunajifunga, Corona ni Adui kwetu”———Rais Samia Bungeni Kenya

“Tanzania sio Kisiwa tunaishi kama sehemu ya Familia ya Jumuiya ya Kimataifa, kupitia Kamati ya Wataalamu niliyoiunda tumeanza mchakato wa kutafakari mbinu zaidi za kukabiliana na Corona”———Rais Samia

“Wakati tunaendelea kusubiri mapendekezo ya Wataalamu (Kamati ya Corona) tahadhari zote ikiwemo kusitisha safari kwenye maeneo yenye milipuko zinachukuliwa, kwa namna yoyote lazima tushirikiane na Jirani zetu, mapambano ya Corona yatulete pamoja na sio kutufarakanisha”———Rais Samia
20210505_193647.jpg
 
“Rais Kenyatta alipokuwa Tanzania alisitisha kuhutubia ili kupisha adhana (Msikitini) imalizilike, alituachia gumzo na fundisho kubwa la kuheshimu imani zetu”———Rais Samia Bungeni Kenya

“Busara inasema ukiwa Mpangaji mpya lazima ujitambulishe kwa Majirani, nimekuja kuitikia wito wa Kenyatta, nimebaini sehemu kubwa ya ujumbe nilioambatana nao wanajua vichochoro vya Nairobi, wanajua nyama choma inapopatikana, ila kutokana na Corona wameshindwa kujibamba, nina wasiwasi wengine nitawaacha huku”———Rais Samia

“Rais Uhuru Kenyatta ni Mtu wa kutimiza ahadi, ili kuondoa mitazamo hasi tumepanga kukutana mara kwa mara maana Ndugu wanaotembeleana hujenga ukaribu kuliko wasiotembeleana, umbali hujenga mashaka na ukaribu huondoa mashaka” ———Rais Samia
20210505_193913.jpg
 
“Nashukuru kwa kukaribishwa kuhutubia Bunge tena kikao cha pamoja cha Mabunge mawili, najua sio kila Rais anayekuja hapa anapewa hii fursa nimefarijika sana, Tanzania tuna Bunge moja, kwangu ndio mara ya kwanza kuhutubia Bunge lenye chemba mbili, ni heshima iliyoje”———Rais Samia Bungeni Kenya

“Uamuzi wenu wa kunipa fursa hii ni kielelezo cha thamani mnayoupa umoja wetu, namshukuru Kenyatta ni miongoni mwa Viongozi wa kwanza kabisa aliyenipigia simu kunipa pole kwa msiba wa Hayati Magufuli na akaja pia Dodoma kutufariji”———Rais Samia

“Sisi ni Majirani hata wanyamapori wetu ni Ndugu na ni Majirani, kuna wanyama wanakuja kupata mimba Kenya wanazalia Tanzania, ingekuwa wanyama wana Uraia wangekuwa Raia wa wapi?, hata Tausi wetu waliopo Ikulu Tanzania wana Ndugu zao Ikulu Nairobi”———Rais Samia
20210505_194044.jpg
 
Kocha Mecky Mexime leo amesaini mkataba wa miaka miwili kama Kocha Mkuu wa Kituo cha Kukuza Vipaji vya Soka cha Cambiasso Sports Management kilichopo Dar es salaam.

Mexime ameeleza kuwa ameamua kufanya kazi na Cambiasso kwasababu anataka kutuliza Kichwa chake kwasababu Vilabu vya Tanzania baadhi ya Viongozi hawana ueledi wa soka.

“Mimi sasa hivi nimeshaingia Cambiasso nimepumzisha kichwa kwasababu huku kwenye Vilabu vyetu wajingawajinga wengi na ndio mpira wetu sisi unapofeli, sisi walimu wa mpira kuna wakati tunafukuzwa kazi na Watu wajinga tu”———Mexime
20210505_194229.jpg
 
Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA) limemtangaza Kocha Hugo Henri Broos (69), Raia wa Ubelgiji kuwa Kocha wao mpya.

Hugo amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuifundisha Afrika Kusini na anatajwa kuwa atakuwa akilipwa mshahara wa USD 50,000 (Tsh Milioni 115.9) kwa mwezi.

Kocha Hugo aliwahi kuwa Kocha wa vilabu kadhaa Ulaya kama Club Brugge, KRC Genk na timu ya Taifa ya Cameroon, mara ya mwisho 2019 alikuwa Kocha wa muda wa KV Oostende.
20210505_194433.jpg
 
“Kuhusu hayo mahindi ambayo yamelala hapo mpakani (mwa Kenya na Tanzania), Waziri nakupa wiki mbili, yote iwe imefunguliwa (Malori yaruhusiwe kupita) na maneno yaishe, hakuna haja ya kuumiza Watu wetu jameni au ni namna gani?”———Rais Kenyatta mbele ya Rais Samia kwenye Kongamano la Wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania nchini Kenya leo
20210505_194547.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom