The Bunyadi ni mgahawa wa chakula uliokuwepo huko London Uingereza, ulianzishwa mwaka 2016. Baada ya miezi miwili tu ukafungwa kutokana na kuzidiwa na wateja, watu walikuwa ni wengi sana. Banyadi ni neno la kihindi lenye maana ya asili.
Kila mteja anaeingia kwenye mgahawa huu anatakiwa kuwa uchi wa mnyama kama alivyozaliwa. Ukiwa ndani ya mgahawa huu ni marufuku kuwa na simu na pia ni marufuku kupiga picha.
Mmiliki wa mgahawa huu Sebastian Lyall alisema kuwa siku chache baada ya kuufungua mgahawa huu zaidi ya watu 25,000 walikuwa wamesha weka oda ya kula hapo, na baada ya kufungwa kulikua na oda za watu 46,000 zimebaki kupata chakula hapo, taarifa zinasema kwamba walifunga ili kutanua zaidi mgahawa huo kwakua ulionekana kuzidiwa na idadi ya watu.
Mteja akishafika mgahawani hapo anaelekezwa na walinzi katika chumba maalumu ambako anaenda kuvua nguo zake alafu anarudi kuagiza chakula. Bei ya chakula ilikuwa inafika hadi Tsh 200,000=.
View attachment 1767740