Makapuku Forum

Makapuku Forum

“Naomba TAMISEMI mkakusanye mapato na matumizi yakafuate sheria na kanuni, nimemleta Mwana-Mama madhubuti (Ummy Mwalimu) nimempa Katibu Mkuu mzuri na Wasaidizi ni imani yangu kuwa kazi itafanywa”———Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi wapya Ikulu Dar es saalam mapema leo

“TAMISEMI mbali na majukumu mengine mna jukumu la elimu na afya, Shule za Sekondari za Wanawake zina bajeti maalum naomba mkasimamie, tunatarajia kujenga Shule 26 mpaka 2025 naomba hili likatimie pamoja na kuendelea kujenga Hospitali za Wilaya”———Rais Samia

“Natambua kuna Walimu wengi tu karibu Elfu 6 au zaidi ambao wameacha kazi, wamestaafu, wamefariki n.k na kunahitajika wakuziba nafasi, Utumishi mko hapa na TAMISEMI mkalisimamie, Walimu Elfu 6 wapatikane haraka ili wakawatumikie Watanzania”———Rais Samia

“Kuna ajira mpya za Madaktari upande wa afya, tumemaliza Hospitali na Vituo vingi, Bajeti ya mwaka huu ni kuweka vifaa na Watumishi kwahiyo Utumishi na TAMISEMI mkalisimamie hili la Watumishi na vitendea kazi kwenye huduma za afya”———Rais Samia
20210406_174933.jpg
 
“Kuhusu suala la mabando kulizuka rabsharabsha juzi hapa, Wananchi wakapiga kelele mkalituliza, kalifanyieni kazi lisizuke namna ile mpo mnaangalia hawa Watu wanakuja tu na mambo yao mpaka Wananchi washtuke na nyie ndio mnashtuka, kakaeni nao”———Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi Ikulu Dar es salaam leo
20210406_175225.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom