Makapuku Forum

Makapuku Forum

20210406_094440.jpg
 
“Wizara ya Mambo ya Nje mnafanya kazi kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mnajua kwamba ina pande mbili za Muungano, naomba akili zikae hivyo kwamba nyinyi mpo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hili ni kwa Mawaziri na Makatibu Wakuu wote”———Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi wapya Ikulu Dar es salaam leo

“Wizara ya Mambo ya Nje mna kazi kubwa ya kwenda kukuza mahusiano na Mataifa ya Nje, Waziri (Mulamula) wewe ni hodari sana katika hili ndio maana nikaona nikuteue, wanakusikiliza, umeshafanya kazi nao sana, naomba twende tukaweke mahusiano mazuri na Mataifa ya Nje”— Rais Samia
20210406_150335.jpg
 
“TRA agizo langu kwenu ni kuacha matumizi ya ubabe na mabavu kwenye kukusanya kodi haisaidii, mtakwenda mtambinya Mtu, mtamkamua, mtamtisha na kupiga uhujumu uchumi anaogopa kwenda Jela atajikwangua atalipa lakini unaua biashara anafunga, kesho nani anakulipa kodi?”——-Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi wapya Ikulu Dar es salaam leo
20210406_150610.jpg
 
“Suala la Covid 19 nafikikiria niunde Kamati ya Wataalamu waliangalie kwa upana wake kitaalamu halafu watushauri Serikali, halifai kulinyamazia aidha kulikataa au kulikubali bila kufanya Tafiti za kitaalamu”———Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kuwaapisha Viongozi Ikulu Dar es saalam leo

“Tutaunda Kamati ya Wataalamu kuhusu Covid 19 watuambie kitaalamu hayo yanayopendekezwa na Ulimwengu kuja kwetu yapoje, hatuwezi kujitenga tu kama Kisiwa na hatuwezi kupokea yanayoletwa bila kuweka cha kwetu, bila kufanya utafiti wa kwetu”———Rais Samia

“Rais Kikwete alituambia akili za kuambiwa changanya na zako, tuweke na zetu tuwe na msimamo maalum unaoeleweka, sio tunasoma tu mambo ya Covid 19 Ulimwenguni, Tanzania deshi deshi deshi haieleweki, tueleweke kama tunakubali au tunakataa”———Rais Samia
20210406_151553.jpg
 
Attachments

  • 20210406_151553.jpg
    20210406_151553.jpg
    33.7 KB · Views: 6
“Suala la Covid 19 nafikikiria niunde Kamati ya Wataalamu waliangalie kwa upana wake kitaalamu halafu watushauri Serikali, halifai kulinyamazia aidha kulikataa au kulikubali bila kufanya Tafiti za kitaalamu”———Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kuwaapisha Viongozi Ikulu Dar es saalam leo

“Tutaunda Kamati ya Wataalamu kuhusu Covid 19 watuambie kitaalamu hayo yanayopendekezwa na Ulimwengu kuja kwetu yapoje, hatuwezi kujitenga tu kama Kisiwa na hatuwezi kupokea yanayoletwa bila kuweka cha kwetu, bila kufanya utafiti wa kwetu”———Rais Samia

“Rais Kikwete alituambia akili za kuambiwa changanya na zako, tuweke na zetu tuwe na msimamo maalum unaoeleweka, sio tunasoma tu mambo ya Covid 19 Ulimwenguni, Tanzania deshi deshi deshi haieleweki, tueleweke kama tunakubali au tunakataa”———Rais Samia
20210406_151625.jpg
 
“Najua TAMISEMI ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi na hiyo kazi itafuata hivi karibuni (Uteuzi na Utenguzi), ili safu itimie na kazi iende ikafanywe....Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Kazi Iendelee)”———Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi wapya Ikulu Dar es salaam leo
20210406_163832.jpg
 
“Wawekezaji wanalalamika sana kumekuwa na urasimu mkubwa Tanzania, kodi kwa Wawekezaji hazieleweki, napokea taarifa kutoka kwa Wasaidizi wangu, Wafanyabiashara wanataka kuniona niwahakikishie kama watafanya kazi kwa utulivu ili warudi Tanzania”——-Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi wapya Ikulu Dar es salaam leo

“Wawekezaji wanataka kuja Tanzania lakini kwa mambo yetu wanakimbia, tuvute tena uwekezaji, tupate ajira,fedha izunguke,uchumi ukue, nikiwa Makamu wa Rais kuna Mwekezaji alikuja, sijui alitishwa nini!, nadhani kaambiwa tutakupiga kosa la uhujumi uchumi, akaondoka”———Rais Samia

“Vibali vya kazi vimekuwa janga, wanaosimamia vibali vya kazi wamejigeuza Miungu Watu , wamegeuza mradi, Mtu anawekeza mnalazimisha aweke Mtanzania, kila Mwekezaji ana haki ya kuweka Mtu anayemuamini yeye kwanini umlazimishe?, mtende haki”———Rais Samia

“Tunataka Wawekezaji wa-enjoy Tanzania, Makampuni yanafungwa Ndugu zangu sio uongo, tukiweka vikwazo tunawarudisha nyuma, wakiondoka uchumi wetu unashuka, ajira zinapungua na mzunguko wa pesa unapungua na hiki ndio kilio kikubwa cha Watanzania kuwa mifuko mitupu”———Rais Samia
20210406_164007.jpg
 
“Mkeyenge nimekuteua kuwa Mkuu wa Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), ulikuwa TASAC unaijua vizuri karekebishe madudu yenu, moja kubwa ambalo limenichukiza sana kwa mwaka mmoja mmefanya vikao 23 vya Bodi na mmetumia karibu Milioni 600 na kitu kwa vikao vya Bodi tu”———Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kuwaapisha Viongozi wapya Ikulu Dar es salaam leo

“Mkeyenge ni Kijana nimekunyanyua wewe ni Kijana ukafanye kazi Wakala wa Meli (TASAC), hapa nitatumia ule msemo wa Aweso, wewe ni Kijana Mimi ni Mama ukinizingua tutazinguana, kafanye kazi pale na sio kwenda kunyanyua mabega kwa wenzio”———Rais Samia Suluhu
20210406_151625.jpg
 
“Mirerani tumejenga ukuta, kuta la kwelikweli tukaweka na Majeshi, lakini Madini yanatoroshwa kama mwanzo, tukibahatika kuliona linaoneshwa hili hapa, piga picha, bonge la Tanzanite, tunajua mabonge mangapi yamepitishwa chini kwa chini yakatoka?, hatujui”———Rais Samia

“Ndani ya Mirerani kuna vitaru, kitaru C kimewekwa akiba lakini sasa kimeanza kuvamiwa, nataka niseme sitaki kuona mkono wa Mtu kwenye kitaru C, walioanza kugawa vitaru kwenye hilo eneo acheni kina matumizi yake”———Rais Samia

“Mirerani tuongeze ulinzi na ulinzi wa pale sio ulinzi wa mabunduki ya CDF, mnajua wenyewe jinsi ya kuwalinda Wachimbaji wenu wasitoroshe Madini, CDF analinda juu Watu wanatorosha chini ya ardhi wanatokea huko, mkapasimamie vizuri”———Rais Samia
20210406_172347.jpg
 
“Tumezoea tunapokwenda kwenye ziara Mikoani na Wilayani, tunapokewa na mabango ya Wananchi wakilalalimikia kero mbalimbali na mabango yale sio mambo ya kushughulikiwa ngazi za juu, naomba tunapokuja Mimi, Makamu wa Rais, tukikuta bango iwe mambo ya Kitaifa"———Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi wapya Ikulu Dar es salaam

“Nataka niseme tukikuta bango moja aidha Mkurugenzi au Mkuu wa Wilaya umekwenda na hii haina maana mkazuie Watu kuandika kero zao, kero za Wananchi mkashughulikie na tukikuta malalamiko kwamba mnawafinya wasiseme hivyohivyo tutawashughulikia”———Rais Samia
20210406_172547.jpg
 
“Mkeyenge nimekuteua kuwa Mkuu wa Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), ulikuwa TASAC unaijua vizuri karekebishe madudu yenu, moja kubwa ambalo limenichukiza sana kwa mwaka mmoja mmefanya vikao 23 vya Bodi na mmetumia karibu Milioni 600 na kitu kwa vikao vya Bodi tu”———Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kuwaapisha Viongozi wapya Ikulu Dar es salaam leo

“Mkeyenge ni Kijana nimekunyanyua wewe ni Kijana ukafanye kazi Wakala wa Meli (TASAC), hapa nitatumia ule msemo wa Aweso, wewe ni Kijana Mimi ni Mama ukinizingua tutazinguana, kafanye kazi pale na sio kwenda kunyanyua mabega kwa wenzio”———Rais Samia SuluhuView attachment 1745069

"Wewe kijana mimi mama, ukinizingua tunazinguana"

Rais wa JMT
Samia Suluhu Hassan
 
“Wizara ya Habari, nasikia kuna Vyombo vya Habari mmevifungia, sijui Viji- TV vya mikononi vile, vifungulieni lakini wafuate sheria na miongozo ya Serikali, tusiwape mdomo wa kusema tunabinya Uhuru wa Vyombo vya Habari, tusifungie tu kibabe”———Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi Wapya leo Ikulu Dar es salaam
20210406_173648.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom