Makapuku Forum

Mitano tena
kwako mama D!
 
Wachezaji watano wa Timu ya Taifa Benin waliosababisha mechi kati yao vs Sierra Leone kuahirishwa kwa kudaiwa kukutwa na maambukizi ya corona, wamepimwa kwa mara nyingine wakiwa Uwanja wa Ndege na kugundulika hawana corona (negative).

Benin waligoma kucheza vs Sierra Leone baada ya kudai kuwa Sierra Leone imefoji matokeo ya corona ya Wachezaji hao ili wakosekane kwenye mechi ili Sierra Leone ishinde kirahisi lakini hata hivyo mechi hiyo iliahirishwa hadi June.

Hii sasa imekua kama tabia kwa baadhi ya Timu Wenyeji Afrika kutumia kigezo cha Wachezaji kukutwa na corona ili kudhoofisha Timu ngeni, Uganda wakiwa Malawi walikutana na kesi kama hii lakini baada ya mvutano baadae Wachezaji hao waliruhusiwa kucheza.
 
Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dr. Bashiru Ally akiwasili Bungeni leo kwa ajili ya kuapishwa baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan jana kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku nafasi yake ya Ukatibu Mkuu Kiongozi ikichukuliwa na Balozi Hussein Kattanga.
 
Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Liberata Mulamula akiingia katika VIwanja vya Bunge, Mulamula ameteuliwa jana kuchukua nafasi ya Kabudi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
 
Waziri Mteule wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Liberata Mulamula akila kiapo cha uaminifu Bungeni leo baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu jana kuwa Mbunge.
 
Naibu Waziri Mteule wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mbarouk Nassor akila kiapo cha uaminifu Bungeni leo baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu jana kuwa Mbunge.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…