Makapuku Forum

Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Dr. Donald Wright kwa niaba ya Serikali na Watu wa Marekani amesaini kitabu cha maombolezo ya Hayati Dr. Magufuli kilichopo Ukumbi wa JNICC, amemuelezea Dr. Magufuli kama Mtu aliyeipenda Nchi na kuhamasisha Watu kuboresha jamii zao.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuongoza maziko ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dr. John Pombe Magufuli yatakayofanyika kesho March 26, 2021 katika eneo la makaburi ya Familia lililopo nyumbani kwake, Chato.

Waziri Jenista Mhagama amesema taratibu za maziko zitafanyika kuanzia alasiri baada ya kumalizika kwa Misa itakayofanyika kwenye Uwanja wa Magufuli———“mwili utaondolewa Uwanjani kuanzia saa 8 mchana na kupelekwa nyumbani kwa ajili ya taratibu za maziko”

Amesema Misa hiyo itaongozwa na Askofu wa Jimbo la Rulenge, Severine Niwemugizi atakayeambatana na Maaskofu wengine zaidi ya watano kutoka Kanisa Katoliki.

Mapema kuanzia saa 1:30 asubuhi kutakuwa na Misa fupi ya Familia itakayofanyika katika kanisa lililojengwa na Hayati Magufuli, lililopo jirani na nyumbani kwake, kisha mwili utapelekwa uwanjani kwa ajili ya Misa kuu, itakayofuatiwa na salamu kutoka makundi mbalimbali.
 
Waziri Jenista Mhagama amesema Misa Kuu ya kumuaga Hayati Dr.John Pombe Magufuli kesho kwenye Uwanja wa Magufuli, Chato itaongozwa na Askofu wa Jimbo la Rulenge, Severine Niwemugizi atakayeambatana na Maaskofu wengine zaidi ya watano kutoka Kanisa Katoliki.
 
“Nimewasili Chato na kutoa heshima zangu za mwisho kwa Hayati Rais John Joseph Pombe Magufuli. Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Apumzike kwa amani, Amina”-
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…