"Kuanzia Juzi hata leo asubuhi nimeona Watanzania wenzetu wenye husda, tena hawako ndani ya Nchi wako huko, wanashawishi Vyombo vya Kimataifa viseme ‘Rais wa Tanzania anaumwa,kajifungia’, tena hawako hapa, wapo huko, tulioko ndani tuko kimya, ni husda”-Waziri Mkuu Majaliwa akiwa Njombe leo
"Watanzania mtulie uongozi wenu upo,Rais Magufuli anaendelea vizuri, kumzushia ugonjwa ni chuki tu, inawasaidia nini?, ‘atoke’, atoke aende wapi?, ‘aje’ aje afanye nini?, umeshamkuta Rais siku moja anazurura kariakoo?, Rais ana mipango yake ya kazi sio Mtu wa kuzurura”-MAJALIWA
"Juzi tu Rais alikuwa Chato akatoka akaenda Kahama, Tabora, Dodoma, akarudi DSM, juzi kaapisha mnataka tena azunguke Nchi nzima, sisi tunafanya nini?, nini umuhimu wa kuwa na Wasaidizi!, azunguke yeye tena Nchi nzima kweli?”