Rais wa Marekani Joe Biden amewarudisha kwenye Makazi yake binafsi yaliyopo Wilmington, Delaware Mbwa wake wawili ambao alihamia nao Ikulu baada ya mbwa hao uanza tabia ya kuwarukia, kuwafokea na wakati mwingine kuwang’ata Walinzi wa Ikulu.
Mbwa hao wenye asili ya kijerumani aliwachukua mwaka 2018 kwenye kituo cha kufugia Wanyama na kuanza kuishi nao, mmoja anaitwa Major na ana umri wa miaka mitatu na mwingine anaitwa Champ mwenye miaka 14.