Makapuku Forum

Makapuku Forum

Polisi Nchini Marekani wamesema wamepata taarifa za ujasusi za kuwepo kwa njama ya kuvamiwa tena kwa majengo ya Bunge la Marekani maarufu kama Capitol mjini Washington.

Taarifa hizo za ujasusi zinatokea takriban miezi miwili tu baada ya Wafuasi wa aliyekuwa Rais Donald Trump kuyavamia majengo ya Bunge hilo ili kujaribu kulizuia Bunge kuthibitisha ushindi wa Rais wa sasa Joe Biden.

Tishio la uvamizi huo linahusishwa na Wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia, hasa wanaotokea kwenye kundi la QAnon linalohusishwa na imani ya kishirikina na ambalo linaamini kuwa Trump atarudi tena madarakani.

Tangazo hilo linatokea katika wakati ambapo Polisi wanaolinda majengo ya Bunge wamekosolewa kwa jinsi walivyoshughulikia uvamizi wa majengo hayo January 06,2021.
20210304_121708.jpg
 
Polisi katika Kaunti ya Kirinyanga Nchini Kenya wanamshikilia Mwalimu wa Karoti Girls High School kwa kumshambulia Mwalimu mwenzake kwa panga chanzo kikiwa ni kumgombea Mwalimu wa Kike aliyefika Shuleni hapo kwa ajili ya mafunzo ya ufundishaji (Field).

Polisi wamesema Mtuhumiwa anashikiliwa Wang’uru Police Station na atafikishwa Mahakamani kwa kosa la kujaribu kuua huku Mwalimu mwingine Alfose Orina akiwa hoi kitandani katika Hospitali moja binafsi eneo la Mwea.

“Tumebaini kuwa Walimu wote wawili walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mwalimu wa kike aliyefika Shuleni siku za karibuni kwa ajili ya mazoezi ya kufundisha kwa vitendo (Field) akitokea Chuoni”- Polisi

Kufuatia tukio hilo Mamlaka za Kenya zimewataka Walimu kuwa mfano mzuri kwa Wanafunzi badala ya kuendekeza tabia za ajabu.
20210304_122107.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa, Said Mtanda @said_mtanda ameiomba kibali Wizara ya Maliasili na Utalii cha kuwavua Mamba ambao wamezaliana kwa wingi katika Ziwa Tanganyika na kuhatarisha maisha ya Wananchi wanaoishi katika Vijiji vilivyopo mwambao wa Ziwa hilo hasa Mpenge, Kabwe, Kamchui na Kalila.
20210304_122332.jpg
 
“Tanki kubwa la maji Lita Milioni 15 la Wilaya ya Kigamboni, Dar Es Salaam, kazi ya kumwaga zege ikiendelea, kazi hii inafanyika kwa haraka na viwango na spidi tuliokubaliana kwenda nayo ili Watanzania wapate maji safi, salama na yenye kutosheleza”- Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
20210304_122549.jpg
20210304_122521.jpg
 
“Mtoa huduma atatoa fursa kwa Mtumiaji wa huduma za Mawasiliano kuchagua na kujiunga na vifurushi visivyokuwa na ukomo wa muda wa matumizi vitakavyopatikana kwenye Menu kuu na watatumia jina linalofanana kwa vifurushi hivi ili vitambulike”- TCRA

“Mtoa huduma ataweka utaratibu wa kumwezesha aliyejiunga na kifurushi chochote kuendelea kutumia muda au uniti za kifurushi zitakazokuwa zimesalia ndani ya muda wa matumizi uliowekwa kwa kununua tena kifurushi hichohicho kabla ya kumalizika kwa muda wake”-TCRA


Aliyeelewa atanielewesha
20210304_122819.jpg
 
“Katika utekelezaji wa kanuni ndogo za vifurushi ambao utaanza Aprili 02, 2021, vifurushi vinavyotolewa kwa Mtumiaji havitaondolewa, havitarekebishwa au kubadilishwa ndani ya miezi mitatu baada ya kuidhinishwa”- TCRA

Haya ndio majibu yao ya miezi 3
20210304_122819.jpg
 
“Mtoa huduma atatakiwa kutoa taarifa kila wakati matumizi ya kifurushi yatakapofikia, kwa mfano matumizi yakifikia 75% wakujulishe kuwa ‘sasa umefikia 75%’ na kabla ya kuisha wakujulishe na pia kitakapomalizika kabisa kwa 100% wakuambie ‘sasa kifurushi kimeisha’, hii ni kwa vifurushi vya muda wa maongezi, data na SMS”- TCRA
20210304_123327.jpg
 
“Mtoa huduma ataweka utaratibu au mfumo wa kumwezesha Mtumiaji wa huduma kuhamisha uniti za kifurushi kwenda kwa Mtumiaji mwingine ndani ya mtandao wake kwa masharti ya kiasi cha chini kuhamisha kitakuwa 250 MB”- TCRA

Hapa kidogo nimewaelewa
20210304_123454.jpg
 
Baada ya uwepo wa malalamiko ya vifurushi kutoka kwa Watumiaji wa simu, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepitisha mabadiliko ya kanuni ndogo za vifurushi ikiwemo kumruhusu Mteja kuhamisha uniti za kifurushi kwenda kwa Mtu mwingine.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Eng. James Kilaba amesema dhumuni la kupitisha kanuni hizo ambazo zinaanza April 02,2021 ni kupunguza tofauti kubwa iliyokuwepo kati ya bei ya vifurushi na bei za kutumia huduma bila kujiunga na Vifurushi.

“Mtoa huduma hatotoa huduma za vifurushi bila kibali cha Mamlaka”-TCRA

Hawa tcra hawa kwa hiyo swala la kushusha vifurushi ndio limeshindikana yani najiona kabisa kurudi kwenye kitorch
20210304_123636.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom