Kwa wapenzi wa muziki wa Country, mwezi huu umekuwa mgumu na wenye majeraha makubwa kwanza kwa kuondokewa na nguli Kenny Rogers, mkali wa Luccile na The Gambler ukiacha nyingine nzuri nyimbo na alikuwa mkali wa gitaa.
mwingine ndo kwanza kabla halijatitia naye kafariki kwa changamoto ya corona iliyosababishwa na complication nyingine. Anaitwa Joe Diffie mkali wa Honky Tonk attitude- Honky tonk ni bar ambazo zinakuwa na muziki ndani yake, kwa hapa bongo tungesema ni sehemu ambazo tunapata muziki wa bakulutu, kwa wakazi wa Shinyanga mjini mnanielewa nasema nini.
Nimependa tu nikuburudishe na muziki wa mkali huyu ambaye si wengi tunamjua kivile