It’s furahiday wadau wa Jukwaa hili ninalolipenda na kulifurahia sababu wewe unayesoma kipengele hiki u sehemu yake. Bila wewe basi Jukwaa hili lingekuwa lolote si chochote.
Naweka video hii kwa sababu nayo ilibamba sana kwenye kipengele cha muziki nilichokihudumu mwaka sasa. Burudika na hii ndo last Friday 2018 so let it be an easy one, smile na toa tano kwa utakayekutana naye.
Hivi binamu kwanini lakini kila ninapomgusia binamu Shadeeya tu, basi lazima uchomekee tujungu fulani?! Sisi ni watoto wa mjomba na shangazi binamu...kupeana raha ni ibada, na kufanyiana husuda ni karaha, yenye kuleta balaa!