Unajua kwamba tumbo lako ni moja kati ya viungo mwilini ambavyo hata vikiondolewa mwilini mwako bado utaweza kuendelea na maisha kama kawaida. Kazi kubwa nne za tumbo mwilini ni kukimeng'enya chakula, kutoa kemikali ambazo zinakilainisha chakula, kukifyonza na kukitoa.
Madaktari wanaweza wakaliondoa tumbo endapo ikatokea kansa au ajali. Mwaka 2012, mwanamke mmoja kutoka Uingereza aliondolewa tumbo lake lote baada ya kunywa pombe iliyokuwa na liquid nitrogen. Unaweza ukaondolewa tumbo lako kisha koromeo (oesophagus) lako likaunganishwa moja kwa moja kwenye utumbo mdogo na maisha yakaendelea bila matatizo.