Makapuku Forum

Makapuku Forum

WENGI HATUYAJUI HAYA KUHUSU UKUTA HUU WA CHINA “Great Wall Of China”


1.Ulianza kujengwa miaka 2000 iliyopita, mpaka sasa una urefu wa kilometa zaidi ya elfu sita (6000 km)

2.Ndio Ujenzi pekee wa binadamu ulio mrefu zaidi duniani kote. Wachina walijenga kwa ajili ya usalama wao hasa kujikinga na maadui kutoka upande wa kaskazini.


3.Ukuta huu una upana wa mita tisa tu (30ft) ambayo ni sehemu nzuri ya kutembea kwa miguu na kuna maeneo mengine, ni salama hata kuendeshea gari.

4.Ukuta Huu ulijengwa na watumwa na wanajeshi kwa awamu mbalimbali na zaidi ya watu milioni moja walifariki katika ujenzi huo

5. Ukuta wa china ndio shughuli pekee ya binadamu inayoweza kuonekana kutoka anga za juu. Ila si kweli kwamba wansayansi waliuona ukuta huu kutoka mwezini.
 
6.Katika hatua za mwanzo, Unga wa mchele ulitumika kuunganishia matofali (kama gundi) wakati wa ujenzi

7.Zaidi ya watu milioni 10 hutembelea eneo hilo maarufu kwa utalii

8. Eneo linalotembelewa zaidi na watalii ni eneo la Badaling karibu kabisa na jiji la Beijing. Eneo hilo limejengwa miaka 2000 baada ya kuanza kwa ujenzi huo mwaka 1957.

9.Jina la China lilitokana na sehemu ndogo ya ukuta huo iliyokuwa ikiitwa Qin Shi Huang, ambapo “Qin” inatamkwa “chin”

10. Toroli (Wheelbarrow) liligunduliwa na wachina katika ujenzi wa ukuta huu maarufu duniani
 
PASSWORD 10 ZINAZOIBIWA ZAIDI NA WEZI WA MTANDAONI. KAMA UNATUMIA KATI YA HIZI, BADILISHA!

1.Namba
“123456”, “12345678”, “123123”, 111111, tarehe ya kuzaliwa, 654321

2. Maneno na Namba
“123abc”, “123qwert”, “tarehe ya kuzaliwa + Jina”,

3. Majina
“Jina lako”, “jina la timu yako”, mpenzi wako nk

4. Herufi
“qwert”, abcdef, “qwertyuiop”


5. Maneno maarufu
“iloveyou”, “F**kyou”, “Soccer”, “welcome”, “Princess”, "Password"
 
ULISHAWAHI KUKUTANA NA NYAKATI HIZI KUMI(10) ZA KUUDHI?

1.Uko kwenye daladala, mara ghafla linapita gari la takataka, Harufu inaingia ndani, ukifunga vioo inabaki ndani, ukifungua vioo inazidi kuingia! Mbaya zaidi mko kwenye foleni

2.Unaangalia simu yako mara ghafla inaingia meseji ya kuchekesha, unacheka kwa sauti kubwa, unagundua kila mtu alikuwa kimya na sasa wote wanakuangalia wewe huku wanatikisa vichwa!


3.Uko hotelini au shopping, mara anatokea mtu anakuuliza bei ya vitu akidhani wewe ni muhudumu!



4.Umekutana na mtu hujaonana nae mda mrefu, unataka kumkumbatia halafu yeye anakupa mkono


5.Unataka kumsimulia mtu habari unayohisi ni ya kuchekesha, unamaliza kusimulia alafu yeye hajacheka.. akidhani inaendelea!
 
6.Unamjibu mtu maswali yote, kumbe hakuulizi wewe anaongea na simu!


7.Unampungia mtu mkono mbele za watu, alafu yeye hajibu chochote.... kumbe umemfananisha

8. Unahangaika Kusukuma mlango ili ufunguke kwa sekunde kadhaa baadae unagundua kumbe mlango umeandikwa "pull" yaani Vuta!


9.Unasimulia Kitu katikati ya watu, mara mate yanaruka na kumuangukia mtu wa jirani, na kila mtu ameona....

10. Unasikiliza muziki masikion (earphones), unagundua watu wote wanakuangalia wewe...... kumbe unaimba kwa sauti ya juu... mbaya zaidi unaukosea wimbo
 
6.Unamjibu mtu maswali yote, kumbe hakuulizi wewe anaongea na simu!


7.Unampungia mtu mkono mbele za watu, alafu yeye hajibu chochote.... kumbe umemfananisha

8. Unahangaika Kusukuma mlango ili ufunguke kwa sekunde kadhaa baadae unagundua kumbe mlango umeandikwa "pull" yaani Vuta!


9.Unasimulia Kitu katikati ya watu, mara mate yanaruka na kumuangukia mtu wa jirani, na kila mtu ameona....

10. Unasikiliza muziki masikion (earphones), unagundua watu wote wanakuangalia wewe...... kumbe unaimba kwa sauti ya juu... mbaya zaidi unaukosea wimbo

...kwenye hii ya mlango, mimi ni muhusika kabisa ha hahahhaha, nikikukmbuka najicheka sana sema niliyekuwa naongozana naye alinisaidia kwa kusema jaribu kupull
 
Back
Top Bottom