Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imeichagua Senegal kuandaa michezo ya Olimpiki kwa vijana (Summer Youth Olympic Games) mwaka 2022. Michezo hiyo itafanyika katika miji ya Dakar, Diamniadio na Saly. Nafasi hiyo pia ilikuwa ikiwaniwa na Botswana, Nigeria na Tunisia.
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linalishikilia lori la mafuta la Kampuni ya Oilcom, baada ya kulikamata likisafirisha katoni 2 za pombe kali na vipodozi katoni 15 vyote vilivyopigwa marufuku nchini likitokea Zambiakwenda Dar es Salaam.
Dereva wa gari hilo alikimbia baada ya kusimamishwa, bado anatafutwa.
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho atafanya mazungumzo na Mkurugenzi wa timu hiyo Ed Woodward jijini London kabla ya bodi ya klabu kufanya mkutano wake siku ya Alhamis. (Sun)
United imeendelea kuwa na imani kuhusu mkataba wa mlinda mlango David de Gea ingawa amekuwa akihusishwa kuihama timu hiyo mara kadhaa, De Gea 27, amekuwa kwenye mazungumzo na Manchester juu ya mkataba mpya. (ESPN)
Chelsea inafanya mazungumzo na Antonio Conte kumumalizia malipo ya malimbikizo yake huku kukiwa na taarifa ya kumuandaa kurudi Chelsea, ingawa amekuwa akihusishwa na kujiunga na Manchester United, Real Madrid na Bayern Munich. (Telegraph)
Beki wa Chelsea na timu ya taifa ya England John Terry ameongeza uwezekano wa kuwa kocha wa Aston Villa baada ya Monaco kuingia katika rada za Henry kuwa kocha wao. (Times)
Wachezaji wa Aston Villa wamependekeza jina la John Terry, 37, kuwa kocha wao baada ya kukiongoza kikosi hicho kama Nahodha mkuu alipokuwa anacheza kwenye ligi daraja la kwanza. (Mirror)
Klabu ya Manchester City itakuwa kwenye nafasi nzuri ya kumsanii kwa mara ya pili kinda wa England Jadon Sancho, 18, anayekipiga katika klabu ya Borussia Dortmund baada ya kuonyesha nia ya kumsajili ingawa itatakiwa kutumia pesa kubwa.(Manchester Evening News)
Maneja wa Manchester United Jose Mourinho amepanga kumfuatilia mwenyewe kwa lengo la kumsajili beki wa Fiorentina na Serbia, Nikola Milenkovic, 20, (Telegraf, via Talksport)
Golikipa wa Stoke England Jack Butland, 25, ameachana na wakala wake wa mda mrefu jambo ambalo linaweza kumshuhudia kurejea kwake katika ligi kuu England. (Telegraph)
Klabu ya Manchester United usajili wa dirisha dogo unaweza usifanikiwe sana kutokana na uwezekano wa kuathirika na Brexit, maneno haya aliyasema Profesa mmoja wa michezo. (Manchester Evening News)
Mshambulaiji wa Argentina Mauro Icardi hajaanza bado mazungumzo ya kupata mkataba mpya na klabu yake ya Inter Milan ingawa bado ana mkataba na klabu hiyo, mshambuliaji huyo anaweza kutolewa Milan kwa dau la pauni milioni 96. (Tiki Taka, via Goal)