Nada Zaelnoon Ahamed (raia wa Sudan Kusini) na Mohamed Belal (raia wa Syria) wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam wakisafirisha USD 70,000 na Paundi 3,410 za Sudan bila kufuata taratibu.
Sheria inataka ukiwa na fedha kuanzia USD 10,000 ujaze fomu ya maelezo kuhusu fedha hizo.
Watuhumiwa wote wawili wamezuiwa na hawawezi kuendelea na safari zao kwa ajili ya uchunguzi zaidi na hatua za kisheria zilizopo