Makapuku Forum


..ha hahhahaha, JF kokoro hili, tunajuana na wengine ni marafiki ambao hatujakutana. Yupo mdau mmoja tulikuwa hadi tunatembeleana ofisini, tulikuwa marafiki wazuri na yupo mrembo mwingine yuko sekta ya afya alikuwa ananisaidia sana aisee na ndiyo maana napaheshimu hapa nikijua wapo watu na viatu ila watu wengi kuliko viatu.

Mimi ni kijana fulani hivi wa makamo ila nina mambo ya kizee, si unaonaga hata nyimbo zangu nazosikilizaga. nina mvi za kimaskini na kakitambi ambako kila siku najitahidi kukaondoa kwa kupiga shots za whiskey na bia. oh, karibu Mtwara, ila kwa sasa nipo Lindi kwa muda

 
Hahahahahaha kuku na maharage na nini kingine

..tatizo anko wangu wewe hata ukivibeba havifiki. unakumbuka uliwahi kuhonga kuku wa kienyeji uliyemnunulia aunt yangu? Kuku hakufika wallah ukaishia kutuma picha tu.

Nina hakika aunt yangu hata akikuagiza toothpick utahonga tu, mambo ya ukoo tunajuana anko, Mungu anakuona lakini
 

Binamu ndio mana huwa nasema sikuelewi

Yaan huwa natamanigi sana kukujua

Korosho zangu ndio hutaki kuniletea ndio basi tena
 

Binamu ndio mana huwa nasema sikuelewi

Yaan huwa natamanigi sana kukujua

Korosho zangu ndio hutaki kuniletea ndio basi tena

...korosho uongo dhambi na krismasi imekaribia, nilimpatia anko wangu Lyon Lee azilete alikuja kutembea huku Lindi alikuwa anaenda Songea , alisema alifikisha lakini alisema kwa ukali sana nilipomuuliza kama kakufikishia, nikajua tu tayari mtu kaliwa kwa korosho zako
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…