Makapuku Forum

 
@behaviourist utukome hatutaki kufa bora tubaki na flat zetu
 
UMEBOREKA? SOMA TAFITI HIZI KUMI KUHUSU SIKU YA JUMATATU UBAKI MDOMO WAZI!

Nasikia kitu kibaya zaidi siku ya jumapili ni pale tu unapowaza kesho ni jumatatu tena na unavitu kibao vinakungoja! Haya ni mambo kumi yatakayokuacha mdomo wazi kuhusiana na siku ya jumatatu.

1.Kwa siku ya jumatatu, Asilimia 60 ya watu hupata tabasamu lao la kwanza saa tano asubuhi (Kabla ya hapo kila mtu huwa amenuna!)

2. Asilimia 50 ya wafanyakazi huchelewa kazini siku ya jumatatu kwa kisingizio cha foleni. Pia ndio siku inayoongoza kwa “sicksheet” nyingi zaidi katika wiki.

3.Kwa kiasi kikubwa saa zima la kwanza kazini huwa kazi haziendelei kila mtu hukuuliza weekend ilienda vipi na kuishia kuzungumzia yaliyotokea hapo kabla, na kazi hufanyika kwa masaa machache zaidi kuliko siku zingine
 
4. watu wenye umri wa miaka 35 mpaka 50 wako kwenye hatari kubwa sana kupata matatizo ya moyo ikiwemo kiharusi siku za Jumatatu!

5. Kwa mujibu wa wataalamu wa saikolojia, Watu wengi zaidi hujiua siku ya jumatatu kuliko siku nyingine yeyote katika juma

6. Siku hii ya jumatatu, ndio siku inayoripotiwa kupata nvua kidogo zaidi kuliko siku nyingine! Wengi huamini hili linatokana na uharibifu wa hali ya hewa unaofanyika mwishoni mwa wiki!

7.Licha ya kuchukiwa na watu wengi, jumatatu ndio siku bora zaidi kununua gari na bidhaa zingine! Hii ni kwa kuwa wauzaji wengi huwa wametumia kiasi kikubwa cha fedha wikendi na jumatatu huwa na wateja wachache zaidi hivyo ni rahisi kupunguziwa bei!
 
8.Kuamka siku za jumatatu huwa kitu kigumu zaidi kukumbana nacho, usingizi huongezeka kadri muda wa kazi unavyokaribia

9. Kazi ulizoacha kiporo siku ya ijumaa huonekana ngumu zaidi ya kawaida na shinikizo kutoka kwa wakubwa zako huongezeka!

10. Jinsi ya kuepuka haya, lala mapema siku ya j’pili, andaa nguo utakayoivaa mapema, andaa vitu utakavyobeba mapema, weka malengo kadhaa ya kutimiza siku ya jumatatu!
 
MAMBO 10 YAKUSHANGAZA KUHUSU WATU WANAOTUMIA MKONO WA KUSHOTO



Watu maarufu

1.Mtu maarufu zaidi Duniani Barack Obama na Bill Clinton raisi wa zamani wa Marekani

2. Tajiri wa Dunia Bill Gates

3. Mwanamke mwenye mafanikio zaidi duniani Oprah Wilfrey

4. Mfalme wa hiphop duniani Eminem

5. Msanii mwenye wafuasi wa kike wengi zaidi duniani Justin Beiber hutumia Kushoto Pia

6.Rafael Nadal Mkali wa Tennis hutumia mkono wa kushoto


7. Wanasoka Lionel Messi, Maradona, Ryan Giggs robin van Persie, ribery na wengine wengi.

8. Muigizaji Maarufu zaidi wa Kike Hollywood Angelina Jolie

9. Lady gaga anatumia mkono wa kushoto

10. Mabondia Mike Tyson, Manny Pacquiao, na Oscar De La Hoya wanatumia mkono wa Kushoto
 
Maajabu Yao
1.Kucha zao za kushoto hukua kwa haraka zaidi ya zile za kulia

2.Wana uwezo wa kufanya kazi za kibunifu zaidi kiliko wenye mkono wa kulia

3.Huchora maumbo yanayogeukia upande wa kulia

4. Hutumia zaidi upande wa kulia wa ubongo, na wengi wao hupenda pombe kwani pombe huchukua muda mrefu zaidi kuathiri upande wa Kulia wa Kichwa Kuliko Kushoto

5. Wanauwezo zaidi wa kufikiria. Huwa na uwezo wa kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja (multitasking).

6. Hupona ugonjwa wa kiharusi(stroke) kwa haraka zaidi

7.Huchelewa Zaidi kubalehe kulinganisha na watoto wanaotumia mkono wa kulia

8.Asilimia 80 ya watu hawa huwa jinsia ya kiume.

9. Watu saba kati ya kumi wanaotumia mkono wa kushoto, huwa na “allergy” ya kitu angalau kimoja


10. Hufariki mapema zaidi kuliko watu wanaotumia mkono wa kulia (miaka 9-10 kabla)
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…