Makapuku Forum

Makapuku Forum

TUOMBE:Baba yetu na Mungu wetu asante kwa ajili ya jumapili ya leo tarehe 30 Septemba 2018Tunashukuru umetuamsha salama ..Asante kwa ajili ya wote wanaotuzunguka wamekuwa baraka kwetu na Asante kwa ajili ya maisha yetu na imani yetu kwako Roho Mtakatifu kaa nasi endelea kutuimarisha.Tusamehe Baba kwa kila ambalo tumeenda kinyume na mapenzi yako uturehemu Tunaomba jumapili ya leo ikawe ya baraka tuingiapo na kutoka kila tutakapoabudu onekana katika ibada zote Baba tutoke tukiwa tumepokea yote uliyotuandalia..tunaomba wabariki watumishi wa Mungu wakatumiwe vyema na Roho wako Baba.ponya wagonjwa,fariji wafiwa ..wape tumaini wajane,wagane na yatima ..tumaini liwe kwako tu Mfalme wa Amani.Tunakabidhi kila tunalopitia katika maisha yetu Baba tunajua kwako liko jibu.Bariki kazi za mikono yetu na Bariki sadaka zetu za leo zote uzitakase ziwe njema machoni pako.Endekea kuwaongoza watoto wetu na wajukuu wetu waendelee kukutafura kwa bidii kukupenda na kukutumikia tunakabidhi maisha yao ,njia tao,mawazo yao na haja za mioyo yao ziwe kwako .Endelea kuimarisha familia zetu imarisha upendo na mshikamano na Baba tujengee tabia ya kukuitankwa kila tunalopitia tutende kwa utukufu wa jina lako takatifu.Tunaomba yote katika jiba la Yesu Kristo Amen.
JUMAPILI NJEMA YA BARAKA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE
Amen
 
Kwa kawaida tunadhani kuwa sehemu ambazo zinapewa ulinzi mkubwa katika nchi yoyote ni Magereza, Ikulu na Benki ingawa zipo sehemu nyingine ambazo zinalindwa sana duniani.

Leo nimekutana na list ya sehemu saba ambazo zinalindwa zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote duniani.

1: Benki ya Federal Reserve

Hii ni Benki iliyopo katika jiji la New York, Marekani ambayo inatumika kuhifadhi zaidi ya 25% ya dhahabu zote duniani. Benki hii ni moja kati ya sehemu zenye ulinzi mkali zaidi duniani ikiwa imejengwa kwa urefu wa futi hamsini kutoka usawa wa Bahari na inalindwa na zaidi ya wanajeshi 5,000.

2: Jumba la Greenbrier

Jumba hili linapatikana katika mji wa Virginia, Marekani ambapo unaambiwa linatumika kuhifadhi vifaa vya nyuklia vya Marekani. Unaambiwa katika jumba hili ndipo viongozi wa juu wa serikali na kijeshi hufanyia mkutano na kuamua wapi watashambulia.
 
3: Mpaka wa Korea Kusini na Korea Kaskazini

Huu ni mpaka ambao unazitenganisha nchi mbili mahasimu duniani. Ni moja kati ya sehemu ambazo zinalindwa zaidi duniani ambapo kuna zaidi ya wanajeshi 2,000 ambao hufanya doria. Ni vigumu kwa mtu kufika kwenye mpaka huu kwa sababu kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yako.

4: Inapohifadhiwa mitambo ya WikiLeakes

Miongoni mwa sehemu zinazopewa ulinzi mkubwa duniani ni pamoja na mahali panapohifadhiwa mitambo ya kundi la wanahabari wachunguzi ambao hutoa siri za nchi mbalimbali duniani wakiwemo viongozi wakubwa wanaotenda kinyume na taratibu za kiuongozi ikiwa ni pamoja na rushwa na matumizi mabaya ya ofisi. Mitambo hii ipo katika milima ya Sweden ambapo unaambiwa ina uwezo wa kuzuia mabomu ya nyuklia.
 
5: Ghala la Doomsday

Ghala la Doomsday lipo katika Kisiwa cha Spitsbergen, Norway ikiwa ni moja kati ya sehemu zinazopewa ulinzi wa hali ya juu zaidi duniani. Ulinzi unaopewa ghala hili ni kwa sababu ndimo zilimohifadhiwa zaidi ya aina 3,000 za mbegu. Hii ni kulinda dunia iwapo kutatokea vita au majanga ya asili yatayakayosababisha uhaba wa chakula duniani.

6: Area 51

Hii ni moja kati ya sehemu zenye ulinzi mkali zaidi duniani. Ni eneo ambalo hutumika kutengeneza ndege za kivita za Marekani, mabomu ya nyuklia na vifaa vya kiteknolojia vilivyotumika katika safari ya mwezini mwaka 1945.


7: Mlima wa Chuma

Mlima huu upo Pennsylvania, Marekani ambao unatumika kuhifadhi mitambo inayoendesha mitandao ‘internet’. Sehemu hii pia hutumika kuhifadhi data na nyaraka za siri za serikali ya Marekani
 
5: Ghala la Doomsday

Ghala la Doomsday lipo katika Kisiwa cha Spitsbergen, Norway ikiwa ni moja kati ya sehemu zinazopewa ulinzi wa hali ya juu zaidi duniani. Ulinzi unaopewa ghala hili ni kwa sababu ndimo zilimohifadhiwa zaidi ya aina 3,000 za mbegu. Hii ni kulinda dunia iwapo kutatokea vita au majanga ya asili yatayakayosababisha uhaba wa chakula duniani.

6: Area 51

Hii ni moja kati ya sehemu zenye ulinzi mkali zaidi duniani. Ni eneo ambalo hutumika kutengeneza ndege za kivita za Marekani, mabomu ya nyuklia na vifaa vya kiteknolojia vilivyotumika katika safari ya mwezini mwaka 1945.


7: Mlima wa Chuma

Mlima huu upo Pennsylvania, Marekani ambao unatumika kuhifadhi mitambo inayoendesha mitandao ‘internet’. Sehemu hii pia hutumika kuhifadhi data na nyaraka za siri za serikali ya Marekani
Ningependa kujua zaidi kuhusu Area 51...
 
Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na Mexico. Kwa upande wa Africa ni kama; Malawi, Zambia na Botswana. Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania.

Kwa upande wa Tanzania mikoa inayolima nyanya kwa wingi hasa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na biashara ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Iringa (Ilula), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida.

View attachment 881772
Niletee nyanya tenga 1000 hapa Bunju nilishie ng'ombe mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom