Makapuku Forum

Nipo hapa kusema kuwa hatujui kila kitu. lakini kile kidogo ambacho tunakijua ndicho tunachokupa wewe. kwa hio usijikatae katika maisha yako. jikubali kwa kila kitu unachokifanya. kubali mawazo yako.

Utaweza kupata maana utakapo pata kwenye vitabu, kutoka kwa mtu, ndio , huenda ni moja ya makala ikakupa kitu kizuri na ukakifanyia kazi . huenda ndio hii ambayo najaribu kukuweka sawa sasa. ni sahihi , na ni nzuri, kusema kweli. kwa sababu tunachagua msukumo wakati tunapohitaji. tunachukua chenye sababu.

Lakini usitake kusema maisha yako yameharibika kwa sababu umekosana na mwenza wako, umeachwa, umeumizwa. hutakiwi kufikiria kuwa umeharibu maisha yako. badala yake tambua kuwa umejifunza, umepata uzoefu wa maisha. Hujaharibu maisha kwa sababu umecheza kwa usalama. hujaharibu maisha yako kwa sababu umechanua tofauti kuliko unavyoamini. hujaharibu maisha yako kwa sababu umekwisha kutatua.
 
Kwa nini?

Kwa sababu hakuna kitu kama hicho cha kuharibu maisha.

Kusema hivyo ni kujishusha thamani, katika maisha mara milioni.

Nia , ndoto zinabadilika. Na sio tu kwa sababu kitu ulichokitaka kitokee hakikutokea haina maana kwamba maisha yameharibika.

Utakuwepo muda katika maisha yako , wakati ambao utasikiliza maoni ya wengine zaidi kuliko kusikiliza moyo wako mwenyewe. Huo wakati utakuwa kimya badala ya kuongea kwenye akili yako. wakati huo utakosa nafasi . ndipo hapo utakutana na lawama ndani yako.

Kutakuwepo na makosa, na kushindwa. Kwa sababu wewe ni mwanadamu. kwa sababu kuna ubaya na uzuri na hakuna uwezekano wa kujua jinsi gani utaishi maisha yako.
 
Maisha ni yako tu na ndiyo uliyonayo. kuna siku unaweza kujisikia vizuri na kuna wakati utajisikia vibaya. Ni sawa kulia au kuchanganyikiwa wakati mwingine. katika siku ambazo utaona ushindi usio na mwisho , furahia. Jaribu kukumbuka kila kitu ambacho sio cha kudumu milele. Kila kitu kinakuja na kuondoka.

Kitu pekee ambacho kinaharibu maisha yako ni kuamini kuwa umefanya.
 
Nimecheka mm hahah hakuna wa kukuchoka mama

Yaan mm post ikiwa ndefu nakuwa mvivu sana nitasoma page ya kwanza ya pili
 
Ewaaaa hivi safi sana yaani asante sana mamy
 
TUOMBE:

Baba Asante kutuamsha salama tukiwa wazima siku ya leo Tunaomba Toba tusamehe..

Tunajikabidhi mikononi mwako endelea kutupigania Mfalme wa Amani.Tuponye,Tubariki,Tuhuishe.
Tunajikabidhi sisi na kila tunalopitia Baba mikononi mwako..wafariji wafiwa wote wape mahitaji na tumaini wajane,wagane ,yatima watie nguvu waliipondeka mioyo.

Damu Takatifu ya Yesu Kristo inene mema makazini,safarini,katika masomo,kwa watoto na wahitaji wote wakutafute wewe .Hesabu hatua zetu Roho Mtakatifu kaa nasi.Ni katika jina la Yesu Kristo naomba na kuamini Amen

SIKU NJEMA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE
 
Hauzimiiiiiiiiiiiiiiiii
motoooooooo hauzimiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
hauzimiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…