
TUOMBE:
Baba Asante kwa kutuamsha salama siku ya leo
Tunaomba Toba kwa makosa yote tuliyotenda kwa mawazo ,maneno, matendo Uturehemu Ee Baba.
Tunaomba ulinzi wako na Roho Mtakatifu atupe uongozi katika kila jambo siku ya leo.
Tusaidie kusema ndiyo kwa yote yaletayo utukufu,tujalie utu wema ,kiasi na upendo wa kweli.
Tunaomba utupe uponyaji wa mwili na roho na tukuzalie matunda mema.
Wabariki wasafiri nchi kavu,majini na angani tuende na kurudi salama.ponya wagonjwa waliopondeka moyo na wote ambao wanakuita Baba.
Bariki kazi za mikono yetu Mfalme wa Amani.
Tunazivunja na kuharibu kazi zote za shetani zinazorudisha kazi ya Mungu na kuleta maafa na mafarakano..Tujalie Amani ,Upendo,Mshikamano katika kila eneo.
Tunawaombea wafiwa wape faraja idumuyo,tunawaombea wajane,wagane,yatima na wote wenye changamoto wape tumaini Baba.Tunaomba Mapenzi yako yatimizwe na tunaomba yote katika jina la Yesu Kristo Amen
SIKU NJEMA YA BARAKA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE


