Makapuku Forum

Makapuku Forum

Najua unaijua Afrika, naomba leo nikukumbushe haya kuhusu Afrika!

  1. Africa ina Nchi 54, na ina Nchi 1 ambayo haijajitawala yenyewe!
  2. Afrika yote ilitawaliwa isipokuwa Ethiopia na Liberia.
  3. Kabla ya Ukoloni, Afrika ilikuwa na "Vinchi" vingi vinavyofikia 10,000 (states).
  4. Ustaarabu wa Misri ndio Ustaarabu wa kale zaidi duniani!
  5. Barani Afrika, Lugha ya Kiarabu inazungumzwa takribani na watu 170 million, ikifuatiwa na English (130 million), Swahili (100), French (115), Berber (50), Hausa (50), Portuguese (20) and Spanish (10).
  6. Zaidi ya robo ya Lugha za Ulimwenguni zipo Afrika pekee!
  7. Zaidi ya 50% ya Waafrika ni chini ya Umri wa miaka 25.
  8. Wakazi wa Afrika watafikia 2.3 billion ifikapo 2050.
  9. Watu wa Afrika wapatao 25 million wanaishi na HIV! (Hii ni sawa na raia wote wa Sudani Kusini na Rwanda). Nchini Swaziland, katika watu wa4, mmoja ni Mwathirika!
  10. Vita vya pili vya Congo (1998-2006) viliua takribani watu 5.4 million na ndio vita vibaya zaidi baada ya World War II, idadi hii ni sawa na watu wote wa Guinea ya Ikweta, Mauritania, Djibout, Comoro, Reunion, Sahara Magh, Sao Tome na Shelisheli kwa pamoja!
  11. Afrika ina watu wachache wenye kupata huduma ya internet, ni wachache kushinda hata wale wanaopata huduma hiyo ndani ya NY, USA!
  12. Kwa makadirio, 90% ya wagonjwa wa Malaria duniani wapo Afrika!
  13. Jangwa la Sahara ndio Jangwa kubwa duniani. Eneo la Sahara ni kubwa kuliko USA!
  14. Afrika ndio bara lenye joto sana na hasa maeneo ya Kalahari, Sahara na Namib.
  15. Katika Madini yote ya duniani, Afrika inakadiriwa kuwa na 30% tu ya Madini ya Dunia!
  16. Nigeria Ndio Mzalishaji Mafuta anaeongoza Afrika, namba 4 kwa Dunia! Nigeria inazalisha Mapipa 2.2 m kwa siku!
  17. Maeneo ya Miinuko ya Witwatersrand nchini Afrika Kusini imezalisha Nusu ya Dhahabu yote ya Dunia!
  18. Jiji kubwa kabisa Afrika ni Cairo.
  19. Reptilia mkubwa kuliko wote duniani (Mamba) anapatikana Afrika tu!
  20. Treni aina ya Rovos ya nchini Afrika Kusini, ndio treni ya kianasa Zaidi duniani.
  21. Bendera ya Mozambique ina Mchoro wa AK-47. Ni Nchi 2 tu duniani zina bendera yenye picha ya silaha. Nyingine ni Guatemala.
  22. Nchi ya Sudan ina idadi ya pyramids 223, ni mara 2 ya pyramids za Misri.
  23. Afrika ina wazungumzaji wengi wa Kifaranza kuliko Ufaransa!
  24. Taasisi kongwe kabisa ya Elimu duniani ni University of Al-Karaouine, ipo nchini Morocco, ilianzishwa kama madrassa mwaka 859 AD na Fatima al-Fihri.
  25. Kabla ya mpasuko, nchi kubwa kabisa Afrika ilikuwa Sudan, ikiwa na eneo la 967,940 square miles
  26. Mpaka kufikia mwaka 2008, Matumizi makubwa ya umeme yalikuwa ni Afrika Kusini (4,759.5kW/h) na Ethiopia ndiyo iliokuwa na matumizi madogo kabisa (42.3 kW/h).
  27. Umbali Kati ya Afrika na Ulaya kwa kupitia baharini ni 14.3 kilometers, Umbali kati ya DSM na ZNZ ni 110 Km.
  28. Mto mrefu kuliko yote duniani ni mto Nile wenye urefu wa 6,650 kilometers (4,132 miles) na umepita katika Nchi 11!
  29. Afrika ndio Nyumbani kwa Mnyama mkubwa kuliko wote duniani na Mnyama mrefu kuliko wote duniani! Wanyama hao ni Twiga na Tembo!
  30. Mnyama muuaji wa binadamu anaeongoza barani Afrika ni Kiboko na sio Mamba wala Simba!
  31. Mwaka 2010, ilihitajika siku 216 kufungua kampuni nchini Guinea-Bissau na zilihitajika siku 3 tu kufanya kitu hicho hicho nchini Rwanda!
  32. Tanzania, Africa, ndiko kwenye tatizo kubwa la Albinism.
  33. Pamoja na mambo mengine, wakoloni walileta Afrika michezo miwili maarufu Soccer na cricket!
Makapuku nimewakumbusha tu!
Nachukua fursa hii kuwakaribisha Ugali dona, mlenda na Nguruka!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom