
TUOMBE:Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa Majeshi Asante kwa siku takatifu ya leo ya kupendeza Jumapili tarehe 29 Julai 2018..Asante kutuamsha salama.
Tunaomba Toba Mungu wetu ..utusamehe twakusihi.Tunasamehe wote waliotukosea.
Tuongoze siku ya leo ibada zote ukaonekane Mfalme wa Amani
Wabariki watumishi wote wa Mungu wakuhubiri wewe Baba .
Waponye wagonjwa na waliovunjika mioyo.Wafariji wafiwa wagane,wajane ,yatima waweke tumaini kwako.
Wabariki wote wanaofunga ndoa siku ya leo Mungu ukatangulie na uwe nao katika kuweka agano hili wadumu katika upendo.
Asante Baba kwa ajili ya familia endelea kuzibariki.
Asante kwa ajili ya ndugu jamaa marafiki endelea kuimarisha mahusiano yetu na upendo udumu.
Asante kwa ajili ya watoto wetu na wajukuu wa kike na kiume wapiganie Baba katika safari ya maisha waimarishe wadumu katika upendo na mshikamano.
Onekana katika kila familia Mfalme wa Amani na uwe sababu ya furaha idumuyo.
Tunaomba endelea kutupigania Baba mwema ponya kila jeraha na tupe uvumilivu wa kimapendo katika maisha haya yaliyojaa taabu,hofu na mashaka tukuone wewe tu utupaye tumaini.huruma yako Mungu wetu isikome.
Tunaomba yote katika jina la Yesu Kristo Amen.
JUMAPILI NJEMA YA FARAJA NA UPENDO DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE

