Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Maarifa Usiyoyapenda, Usijikweza Pasi Jilinganisha

...hapa ni siasa na maisha, ndo lengo la kipengele hiki. Sitaacha kukukumbusha kuhusu hili. Maamuzi sahihi huja baada ya kuwa umejiridhisha kwa kuwa na taarifa sahihi, ukweli wenye data (facts) na kutambua (appreciate) mawazo mbadala. Unahitaji kutafiti ili uje na maamuzi sahihi na hapa ndipo hoja yangu ya leo ilipo, maarifa usiyoyapenda unayahitaji na ni ugonjwa wa akili kudhani uko sahihi usiwasikilize wengine (belief superiority). Maamuzi ya jamii hufanywa kwa wengi kuchangia mawazo yao na si kikundi cha watu wachahce wanaojiona wana dhamana kuliko wengine. Tafasiri unavyoweza.

Uzoefu na tafiti zinaonesha kuwa viongozi wa serikali yetu wanaojiona wana akili kuliko wengine, wanaojiona mawazo yao yako sahihi kuliko ya wengine, wana hatari ya kufanya maamuzi mabovu kwa sababu hawakutaka kusikia mawazo mengine ambayo yangewawezesha kujifunza na kufahamu mengi. Chukulia mfano wa waziri mmoja ambaye kwa maamuzi yake tu alienda kununua kivuko chakavu kwa mabilioni ya shilingi akakipaka rangi kionekane ni kipya, kilipowekwa baharini mtumbwi ulikuwa na kasi kuliko kivuko 'cha kisasa'.

Kubali kusikiliza mawazo hata ya wanaokupinga, kuna mengi ya kujifunza kwayo. Tafasiri unavyoweza
 
Shikamoooo binamu
Anti yko leo hayupo kapumzishwa
 
Najaribu kuangalia kama maboresho aliyosema Maxence Melo yamefanya kazi hata huku kwa Makapuku
cat_almost.gif
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom