
TUOMBE:
Mungu wetu na Baba yetu Asante kwa neema hii ya kutuamsha salama Jumamosi ya leo tarehe 21 Julai 2018.Tunakushukuru kwa pumzi uliyotupa leo.
Tunaomba Toba kwa yote tuliyokosea kwa maneno,matendo,
mawazo na kutotimiza wajibu.Uturehemu ee Baba.
Tunakushukuru kwa sababu ya zawadi njema ya familia,ndugu ,jamaa na marafiki wote.
Endelea kutukumbatia Baba mwema.
Bariki kazi za mikono yetu.
Ponya wagonjwa na gusa wote waliovunjika moyo.
Wafariji wafiwa,wajane,wagane,
yatima na wenye changamoto mbalimbali. Endelea kuwapigania Mfalme wa Amani.
Asante kwa ajili ya furaha,Amani,Mshikamano katika maisha ya kila siku.Tukumbushe kupenda zaidi,kutoa zaidi,kusamehe zaidi na kuwatendea wema hata maadui kwa ajili yako mwenyewe.
Wabariki wasafiri mahali popote angani,majini,nchi kavu hata kwa miguu waende na kurudi salama .
Tujalie uvumilivu na utu wema na tutende namna tungependa watu watutendee.
Tunaomba yote kwa jina la Yesu Kristo Amen .
JUMAMOSI NJEMA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE.

