Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Kazi Yako Muhimu Kwetu

Masaa ya kiserikali kufanya kazi kwa siku ni 8 (nane) tu na kwa maana hiyo kwa juma zima wengi wetu hufanya kazi masaa 40. Kazi ninamaanisha ni nafasi uliyoajiriwa/kujiari na huendana na malipo mahususi. Natambua kabisa wengi wetu hufanya kazi zaidi ya moja, hakuna ubaya kwa sababu mimi naelezea kazi yako ya msingi inayokulipa mshahara na inakuhakikishia maisha ya uzeeni kama utabahatika kufika huko. Tafasiri unavyoweza.

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamekuja na mengi, kwanza tumeona uzalishaji ukiongezeka kwa kiwango kikubwa sana (efficiency), bidhaa nyingi sana tunaziona sokoni tofauti na wakati mwingine wowote. Huduma nazo zinazidi kuboreka na mtumiaji wa huduma sasa ana uhuru wa kuchagua atumie huduma ipi kutokana na mahitaji yake.

Upo utafiti kuwa baadhi yetu hatuoni kama tunachofanya kwenye makazini kinasaidia jamii (meaningful contribution to our society). Mitandao inawafanya walimu waone kama huduma yao haina nguvu tena madarasani na ulimbukeni wa baadhi ya wanafunzi wanajiaminisha kila kitu kinapatikana 'gugo'. Pamoja na kuwa sasa baadhi ya mataifa yanahama toka kwenye uga wa uzalishaji (production industry) kwenda kwenye uga wa huduma (service industry) bado hakujaondoa ukweli kuwa kazi unayofanya ina nguvu sana katika kubadilisha maisha yangu, ya yule na ya kwako na kinyume chake kwako.
Tia juhudi katika kile unachofanya maana huduma unayotoa inaweza kuonekana moja kwa moja (direct impact) na isioonekana moja kwa moja. Wewe na kazi unayoifanya mnachangia kwa kiasi kikubwa sana kuweka tabasamu usoni kwa kila anayekutana na wewe.
Asante sana binamu yangu
 
Mkuu huku ukinywa bila kulewa ni sawa na kwenda disco bila kucheza

..hata nikinywa fanta passion?

anigif_enhanced-buzz-19308-1373644751-37.gif
 
Back
Top Bottom