Tafasiri Unavyoweza: Elimu Inasafiri Zingatia Machache
Kama kuna kitu huwa napenda kuandika na kujifunza sana ni kile kinachohusu elimu, nina sababu nyingi za kufanya ninavyofanya. Mojawapo kubwa ni kuwa elimu ni mkombozi, inakufungua macho na kuzipa nguvu zako za kimwili nguvu nyingine ya kufanya jambo la manufaa kwako, jamii inayokuzunguka na taifa kwa ujumla. Elimu ni kila kitu na hapa ninaongelea zaidi elimu inayopatikana kwa mtaala maalum na huhusisha mitihani na kupata cheti. Tafasiri unavyoweza
Ni jambo muhimu kuisaka elimu, hili linajulikna na hata kwenye misahafu usemi huu unazungumzwa sana. Elimu ukiipata, maarifa yanaongezeka na uwezekana wa kufanikiwa maishani ni mkubwa, usiidharau elimu ambayo ukihitimu unapewa cheti. Hivi ulishajiuliza kwanini wababe (gangsters)hujichora chata (tattoos) mwilini? Jibu ni rahisi tu, kuonesha kwa wengine namna walivyo wababe na hivyo wewe isake elimu pata vyeti ndo chata zako.
Elimu inasafiri (elimu masafa) kwa sababu sasa huhitaji muda wote kuwa darasani, kuonana na mwalimu. Sasa unapata elimu masafa na maisha yanaendelea. Ukisoma elimu masafa (mfano OUT na vyuo vya nje ya nchi) zingatia mambo yatakayokufanya ufaulu hata kama huonani na mwalimu wako uso kwa uso. Jali ratiba ya kujisome, tenga muda wa kwenda maktaba na wasiliana na mkufunzi wa kozi unayosoma ili akupe mwongozo wa nini ufanye ukamilishe kinachotakiwa. Usione uko mwenyewe, huonani na mwalimu ukadhani ndo muda wa kufanya uzembe (slacker), elimu inayosafiri ina mitihani. Tafasiri unavyoweza.
Nikutakie mapumziko mazuri ya weekend na tukutane tena wiki ijayo panapo majaliwa.