Obe
Platinum Member
- Dec 31, 2007
- 10,324
- 35,842
Tafasiri Unavyoweza: Ziara za Mafunzo, Wanajifunza Nini?
Hakuna ubishi kuwa tunatofautiana uelewa, na muda wa mtu na mtu kuelewa kunatofautiana.Hili la kutofautiana katika kuelewa jambo sio tatizo kwa sababu maana kisifa cha kuelewa ni kuchukuliana sisi kwa sisi (humane, compassionate). Hata hiyo mada yangu leo si hii ya tofauti ya kuelewa jambo na kulifanyia kazi, ninajikita kwenye ziara za mafunzo ambazo ni maarufu sana kwa viongozi wa serikali. Ziara za mafunzo kwa baadhi ya viongozi zipo kwenye mpango kazi na bajeti ya idara/taasisi husika, lazima wakatembee kujifunza. Tunategemea kabisa wakitoka kujifunza basi tutaona kitu kipya wakikileta kwenye jamii yetu. Tafasiri unavyoweza na hasa kama ukiwwa umeona mabadiliko kwa kiongozi unayemuamini kwa sana.
Mawaziri, wabunge na madiwani ni viongozi muhimu kwenye kuhakikisha sera zinatengenezwa kwa kuleta maendeleo na hawa katika kuelewa masuala wanapatiwa ziara kadhaa za mafunzo na kuona (exposure) wengine wanafanyaje kwenye masuala yanayofanana na tunayotaka. Bahati mbaya sana wapo viongozi ambao wamekuwa madarakani kwa miongo kadhaa na wamehudhuria mafunzo karibu kila mwaka, Ajabu sana miongo waliyokaa madarakani imewageuza kuwa waongo na waficha taarifa. Hawaleti mrejesho wa kile walichojifunza na hata wakileta mrejesho huwa ni katika kujinufaisha wao zaidi badala ya umma. Wanajifunza kuhusu maboresho ya huduma za jamii lakini huduma za jamii kwetu bado ni mtihani na wala haziangalii itikadi. Tafasiri unavyoweza.
Hawa wanaopelekwa ziara za mafunzo karibu kila baada ya miaka mitatu wanajifunza nini? Tunategemea waje na jambo jipya la kuboresha maisha ya wengi lakini tunachoona kila wakitoka ziara za mafunzo na nguo mpya wanazaa na wachache wetu tunajiaminisha zira hizi huwa haziwasaidii chochote zaidi ya kuwa mpango kando wa kujipatia pesa wasiyoifanyia kazi. Tafasiri unavyoweza