Makapuku Forum

Makapuku Forum

..
9d98ad95d81fbbca05e9e94006c6fa82.jpg
 
*[emoji524]MAOMBI YA KUOMBA KWA AJILI YA WAGONJWA NA WALIOKATA TAMAA* .
______________________

Inawezekana ukaona kuwa mbona maombi haya yangefaa kuona na mtu moja kwa moja........

Lakini nataka nikutie moyo na kukujulisha kuwa.

" _NENO LA MUNGU HUTUMWA NA LINAPOTUMWA HALIRUDI BURE_

_HAKUNA UMBALI KWENYE MAOMBI_

_
_Kikubwa jenga Imani ya kimaombi kwa AJILI ya kile unachoomba__

[emoji120] *WAPO WATU WAMELALA NI WAGONJWA WANAHITAJI ANGALAU HATA MTU MMOJA WA KUWAMBEA TOBA KWA MUNGU* .

[emoji120] *WAPO WATU NI WAGONJWA NA WANAHITAJI MAOMBI YAKO TU.*

[emoji120] *WAPO WATU WAMEKATA TAMAA* .

_
_Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao_ ._

[emoji365] *Zaburi 107:20*

Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa.

[emoji365] *Zaburi 34:18*
Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

[emoji365] *Isaya 61:1*
Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala.

[emoji365] *Ezekieli 34:4*
Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu.

[emoji365] *Ezekieli 34:16*
,_______________

_Ubarikiwe sana mtu wa Mungu ukipata muda sema na Mungu kwa AJILI ya hili_IJUMAA NJEMA[emoji120]
 
TUOMBE:Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa Majeshi Asante kwa siku ya leo Ijumaa Tarehe 2 Machi 2018 Kwa Upendo Mkubwa na Neema yako Umetuamsha Baba tukiwa wazima wapo wengi walitamani kuiona siku hii ya leo kwa namna mbalimbali hawajaweza Baba Tunasema Asante kwa yote unayotutendea Tunamualika Roho Mtakatifu akae nasi Kutuongoza.

TUNAOMBA Utusamehe makosa yetu tunayokukosea kwa mawazo kwa maneno na kwa matendo na kwa kutotimiza wajibu mbalimbali kwanafasi tulizonazo uturehemu Baba unatufahamu vizuri tuumbie moyo safi tukujue wewe tu

Tunawaombea Wagonjwa wote waguse Baba waponye na wainuke tena kutoka vitanda vya ugonjwa na mauti Watie nguvu wanaoguza wasipungukiwe

Baba tunaombea Familia zetu watoto wetu wake zetu waume zetu wasaidizi wetu majumbani ndugu jamaa na marafiki wakujue wewe tu na kukufuata

Baba walinde wasafiri wote wa majini nchi kavu na Angani Ukawe dereva wa kila chombo Damu yako ya thamani iwafunike.

Bariki kazi za mikono yetu zikapate Baraka yako Mfalme wa amani Utumishi Huduma Masomo mashuleni Ujasiriamali Ajira vibarua na vyote tunavyofanya viwe na Baraka yako iliyo kuu

Baba angalia Wafiwa Wajane Wagane Yatima Wahitaji Wasiojiweza Wenye Uchungu Waliokata tamaa walioachwa waliotelekezwa waliokataliwa wasio na makazi waliopotea warudi makwao wanaotafuta kazi ukawe Mfariji wa pekee ukaonekane kwao Baba leo hii Baba Tukusifu na kukuabudu wewe Mfalme wa Amani Baba Bariki kila tutachogusa siku ya leo Damu Ya Yesu ikaponye kila jeraha

Tunaombea Taifa letu liwe na Amani Tunavunja kila hila za adui katika Taifa letu.

Mahitaji yetu yote yakapate kibali mbele zako.

Baba unatujua vyema Asante kwasababu Utatenda sawasawa na mapenzi yako Amen.

DAMU YA YESU ITUFUNIKE IJUMAA NJEMA
Amen, ubarikiwe mama
 
*[emoji524]MAOMBI YA KUOMBA KWA AJILI YA WAGONJWA NA WALIOKATA TAMAA* .
______________________

Inawezekana ukaona kuwa mbona maombi haya yangefaa kuona na mtu moja kwa moja........

Lakini nataka nikutie moyo na kukujulisha kuwa.

" _NENO LA MUNGU HUTUMWA NA LINAPOTUMWA HALIRUDI BURE_

_HAKUNA UMBALI KWENYE MAOMBI_

_
_Kikubwa jenga Imani ya kimaombi kwa AJILI ya kile unachoomba__

[emoji120] *WAPO WATU WAMELALA NI WAGONJWA WANAHITAJI ANGALAU HATA MTU MMOJA WA KUWAMBEA TOBA KWA MUNGU* .

[emoji120] *WAPO WATU NI WAGONJWA NA WANAHITAJI MAOMBI YAKO TU.*

[emoji120] *WAPO WATU WAMEKATA TAMAA* .

_
_Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao_ ._

[emoji365] *Zaburi 107:20*

Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa.

[emoji365] *Zaburi 34:18*
Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

[emoji365] *Isaya 61:1*
Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala.

[emoji365] *Ezekieli 34:4*
Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu.

[emoji365] *Ezekieli 34:16*
,_______________

_Ubarikiwe sana mtu wa Mungu ukipata muda sema na Mungu kwa AJILI ya hili_IJUMAA NJEMA[emoji120]
Amen, na kwako pia mama
 
Bhasi bwana yaliyotokea yametokea jana na kumekucha salama japo chondechonde naomba maombi yenu kwa mwezi huu yawe juu ya mpendwa wenu binamu yangu Obe make kila kukicha anaibuka na jipya ...binamu nakusalimia sana na nashukuru kwa uliyoyafanya usiku ....

Arsenal kama kawaida kama kawa ...uf soon

Anko, ule usiku wa Arsenal nilikutumia namba lakini ukaipotezea sasa tusilaumiane ikiwa namba imeenda kwa kamanda Mambonow
 
Tafasiri Unavyoweza: Usawa wa Furaha

Wote tunahitaji na tunapenda kuwa na furaha kila siku. Kuitafasiri furaha inategemea utofauti wetu lakini kuna wakati tunakubaliana kuwa kuwa na furaha ni ile hali ambayo binafsi au kijamii unayaona mafanikio (prosperity), kuridhika na kuwa karibu na unayempenda au unaowapenda. Namna ya kuifikia furaha inatofautiana kati ya mtu na mtu. Kwenye taifa, taifa lenye furaha ni lile ambalo wananchi wake wana usalama, tatizo dogo la ajira, huduma bora za kijamii na kiuchumi, miundombinu rafiki kwa kila mtu na zaidi uhuru wa kupata na kutoa maoni. Tafasiri Unavyoweza.

Kwenye mahusiano, iwe ni ndoa/family au kuishi pamoja (cohabiting) furaha inakuja pale ambapo kila mmoja anachangia kiusawa katika kutoa zawadi (rewards) na kuingia gharama (costs) za kuishi pamoja. Kukikosekana zawadi na gharama katika mahusiano basi furaha haitakuwepo kamwe hata kama mtaonekana kukaa pamoja machoni mwa watu wa pembeni. Kila mmoja anapochangia furaha ndani ya mahusiano kuna faida nyingi sana kibinafsi na kwa pamoja. Utegemezi wa mmoja huondoa furaha haijalishi unapendwa au unapenda vipi. Maisha yana milima na mabonde na ukiwa tegemezi sana utaingia gharama ya kutojiamini na matokeo yake ni kutokuwa na kujiamini (unstable self-esteem) pia kujaa wivu wenye sababu ya wewe kutochangia ndani ya mahusiano (feelings of jealousy and or inadequacy).

Kuifikia furaha kuna mchakato na wakati mwingine si rahisi kama unavyoweza kutafasiri kwamba furaha huja kwa sababu ni jambo la asili (natural happiness), inahitaji muda na nguvu kuifikia furaha na kwa pamoja kuifikia furaha ambayo inaweza kuugeuza umaskini kuwa utajiri ni kwa wewe kuchangia asilimia miamoja katika mahusiano yako uliyonayo. tafasiri unavyoweza.

Nikutakie mapumziko mema ya weekend na tukutane tena wiki ijayo, tunza afya yako hii ndo furaha ya msingi.
 
Back
Top Bottom