Makapuku Forum

Makapuku Forum

[emoji524]Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
And whatsoevcer ye shall ask in my name, that will I do, that the Father may be glorified in the Son.

Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

I will not leave you comfortless: I will come to you.

Yohana 14:13:18.
Shalom tuombe lolote kwa jina la YESU KRISTO naye atatusikia..
Ametuahidi hatatuacha yatima yupo kwetu akitusaidia..
Nawatakia ucku mwema Damu ya YESU KRISTO iwafunike mlale salama..
Shalom [emoji870][emoji1327]‍♀[emoji1327]‍♀[emoji176]
 
Tafasiri Unavyoweza: Matatizo Sio Vikwazo, Ni Miongozo

Hakuna siri kwamba tunapitia mambo mengi sana kibinafsi, kijfamilia, na hata kitaifa. Ndiyo, tunapitia mengi mazuri na mengi mabaya yanayotupa ujasiri, huzuni na mengine yanatufanya tukae chini kujiuliza kama njia tunayoenenda nayo ni sahihi. Njia zote tunazotumia kutaka kwenda tunapotaka si zile zilizonyooka pekee, kuna milima na mabonde bila kuyasahau makorongo na mitelemko. Tafasiri Unanvyoweza.

Wengi wetu ni watumiaji wa barabara, na barabara timamu ina alama za kukuongoza mtumiaji uwe unaitumia kwa miguu au kwa vyombo vya moto. Alama hizi kutaja chache ninazozifahamu ni pundamilia, alama ya kusimama na mwendo sahihi unaohitajika. Ndivyo na maisha yalivyo. Kuna alama za kila namna kwenye maisha na hasa ikiwa wewe ndo ushafikia umri wa kujiendesha mwenyewe. Kujiendesha mwenyewe maana yake kuna wakati utahitaji kuendeshana, tafasiri unavyoweza.

Usikwaze na alama za kukusimamisha (stop signs) hizi zipo, ziheshimu. Matatizo yawe ya mahusiano, kikazi, kifamilia, kiuchumi na kiimani kutaja machache ni alama ambayo haipaswi kukusimamisha katika kile unachoamini ni sahihi kwako na afya ya amani yako. Tumia matatizo kama muongozo (guideline) ya kukufanya ukomae na kulifikia lengo unalohitaji kibinafsi, kifamilia na kitaifa. Matatizo hayataisha na ndiyo maana umepewa kichwa chenye ubongo, yatatue uende mbele unapohitaji. Tafasiri Unavyoweza
[emoji122] [emoji122]
 
Muziki: Ubuyu Wa Rangi ya Lipstick

...nimeona nikutaarifu tu mapema ili usije ukasahau na ukadhani mimi nitasahau kukusalimia Kapuku wewe unayelianya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri ya kuwepo. Asante sana mjomba Lyon Lee kwa UF, nikushukuru BlessedHope kwa sala na salamu za upendo kwetu kila wakati unapopata nafasi ya kutushirikisha furaha yako, tunakupenda sana.

Mjomba wangu kakasirika sana wiki hii kisa kalenda kwanini imekomea tarehe 28 tu wakati alikuwa na booking ya tarehe 29/2/2018 na tayari alikuwa keshalipia nauli ya mgeni kuja kumbe kaingizwa jau na aunt yangu alikuwa hana taarifa maana taarifa ataitoa wapi wakati muda wote analamba ubuyu tu wenye rangi rangi iliyofikia hatua ya kutohitaji lipsticktena. Rangi ya ubuyu imekuwa ni mbadala wa lipstick. Hongera ubuyu wa Zanzibar
Muziki sana, kesho ni furahiday kama ulikuwa hujui, tambua sasa na jipange maana kama utaamua kwenda out hata kama umekaribishwa hakikisha una hela mfukoni

Kesho mimi nitachagua songi la kufurahi
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Back
Top Bottom