Makapuku Forum

Makapuku Forum

TUOMBE:Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa Majeshi Asante kwa siku ya leo Ijumaa Tarehe 2 Machi 2018 Kwa Upendo Mkubwa na Neema yako Umetuamsha Baba tukiwa wazima wapo wengi walitamani kuiona siku hii ya leo kwa namna mbalimbali hawajaweza Baba Tunasema Asante kwa yote unayotutendea Tunamualika Roho Mtakatifu akae nasi Kutuongoza.

TUNAOMBA Utusamehe makosa yetu tunayokukosea kwa mawazo kwa maneno na kwa matendo na kwa kutotimiza wajibu mbalimbali kwanafasi tulizonazo uturehemu Baba unatufahamu vizuri tuumbie moyo safi tukujue wewe tu

Tunawaombea Wagonjwa wote waguse Baba waponye na wainuke tena kutoka vitanda vya ugonjwa na mauti Watie nguvu wanaoguza wasipungukiwe

Baba tunaombea Familia zetu watoto wetu wake zetu waume zetu wasaidizi wetu majumbani ndugu jamaa na marafiki wakujue wewe tu na kukufuata

Baba walinde wasafiri wote wa majini nchi kavu na Angani Ukawe dereva wa kila chombo Damu yako ya thamani iwafunike.

Bariki kazi za mikono yetu zikapate Baraka yako Mfalme wa amani Utumishi Huduma Masomo mashuleni Ujasiriamali Ajira vibarua na vyote tunavyofanya viwe na Baraka yako iliyo kuu

Baba angalia Wafiwa Wajane Wagane Yatima Wahitaji Wasiojiweza Wenye Uchungu Waliokata tamaa walioachwa waliotelekezwa waliokataliwa wasio na makazi waliopotea warudi makwao wanaotafuta kazi ukawe Mfariji wa pekee ukaonekane kwao Baba leo hii Baba Tukusifu na kukuabudu wewe Mfalme wa Amani Baba Bariki kila tutachogusa siku ya leo Damu Ya Yesu ikaponye kila jeraha

Tunaombea Taifa letu liwe na Amani Tunavunja kila hila za adui katika Taifa letu.

Mahitaji yetu yote yakapate kibali mbele zako.

Baba unatujua vyema Asante kwasababu Utatenda sawasawa na mapenzi yako Amen.

DAMU YA YESU ITUFUNIKE IJUMAA NJEMA
 
Bhasi bwana yaliyotokea yametokea jana na kumekucha salama japo chondechonde naomba maombi yenu kwa mwezi huu yawe juu ya mpendwa wenu binamu yangu Obe make kila kukicha anaibuka na jipya ...binamu nakusalimia sana na nashukuru kwa uliyoyafanya usiku ....

Arsenal kama kawaida kama kawa ...uf soon
 
...
db4c88993f2fd83aa1d9ab346b79f394.jpg
 
Back
Top Bottom