Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Happy Birthday To You

Ujue nimeandika title kiinglishi na asikufiche mtu hakuna kazi ngumu kama kuanza kutengeneza sentensi kwa kiinglishi. Ni ngumu si kidogo maana kwa sisi tuliosoma shule ambazo kengele ilikuwa ni ringi la tairi la roli tunajuana kabisa kuwa kiingereza chetu kuna mahali hakiko sawa. Na ndiyo maana huwa tunasalimiana kiinglishi na baada ya salamu tu hatuendelei na kizungu, tunarudi mstarini kuhesabu namba labda uwe umechelewa ndo utapewa lile likibao la Swahili speaker. Nakusalimia kapuku mheshimika.

Nilikuwa na wakati mzuri leo na nilichofanya yote niliyotaka kutafanya bila shida asante kwako wewe ambaye hujauliza siku yangu ilikuwaje. Nilikuwa na anko wangu huyu mnayemfahamu tukipanga mipango yangu halali na yake haramu maana unawezaje kupanga kwenda kula kitimoto bila bia. Halali huenda na halali na kamwe haramu haiendi na halali, fanya unachoona ni sahihi kwako, mambo ya halali au haramu subiri siku ya hukumu, wewe ni nani hata useme halali na haramu kwa kila mtu. Toto baya zuri kwa mama yake.

Muziki sasa, jana ilikuwa ni tarehe ya kuzaliwa BlessedHope , niliimiss ila sio kwa makusudi maana mjomba aliniambia tusimsumbue kwa sababu BH yuko kwenye siku yake, nikatulia na ninaamini hata wengi tumeona leo. Tunakupenda BH na Heko ya Kumbukumbu ya Kuzaliwa

 
Muziki wa Mdhamini: Najidhamini kwa Ajili Yako

Unganeni tu na mimi, leo hadi mjue kuwa mimi leo nimedhamiria kikamilifu kumpongeza mama yenu ambaye huwa mnasomaga tule tumaandishi twangu tudogo kwenda kwake.

Huu muziki/wimbo anaupenda nami sitachoka kuucheza hapa tufurahi pamoja..

 
[emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji253][emoji253][emoji253][emoji253][emoji253][emoji253][emoji258][emoji258][emoji258][emoji258][emoji258][emoji258][emoji253][emoji253][emoji253][emoji253] nimemkumbuka mukongo mm jaman angekuwepo kutoa mauwa binamu Mungu anakuona kwa kunipotezea mukongo wa mama
[emoji23] [emoji23] [emoji23] binamu mwenyewe kutoa maua hawezi
 
Tafasiri Unavyoweza: Swali na Masahihisho

Usije ukadhani kuwa kila swali lina hitaji majibu, usitegemee utakutana na hali ya jana kila siku maana jana na leo ni siku mbili tofauti na kwa kuwa ni mbili basi sahau kuona moja jumlisha moja u=inakuwa tatu na si mbili. Kwa kwa kuwa moja na na moja ni mbili na wala si tatu kwa kujumlisha basi hoja yangu ya kutafasiri inasema kuwa si kila swali linahitaji majibu, maswali mengine yanahitaji marekebisho na si majibu.

Unaweza kujiuliza kwanini pamoja na kuwepo kwa rasilimali chekwa kwenye taifa letu bado umaskini uliokithiri unatamalaki na kumea kama uaridi kwenye samadi. Hapa kujiuliza swali ukitegemea majibu ni kujidanganya na kujilisha upepo tu, swali unalojiuliza ni lazima ulirekebishe kwanza, lifanyie masahihisho ndo liwe swali vinginevyo linabaki kuwa ni maneno yenye kiulizo badala ya nukta.

Unajiuliza haki yangu iko wapi, unapoteza muda, haki huletewi kwenye sahani. Fuatilian na ndipo utagundua kuwa unapaswa kutafasiri unavyoweza kila ninachoandika na kila unachosoma maana asubuhi ninatafasiri vingine na mchana nikishiba tafasiri ya asubuhi inabadilika. Tumewaona wanaotaka tuwaombee ilihali hawataki kuwauliza tuwaombee juu ya nini na hapa ndo majibu kabla ya swali. Tafasiri unavyoweza
Sawa na msafiri asafiriye na asijue aendako basi sawa, sio lazima tutafsiri au sio mtaasisi?
 
...nikiweka kwenye bags kuna hatari ya kukutana na mgambo wa jiji wakadhani mimi ni mmachinga. lazima kitu kikae kwenye karatasi yenye mng'aro wa mcharo
Kwenye mng'aro tunawapelekea watoto wanaogradueti, huku ukubwani tunaweka kwenye bahasha tu maana hatupangiani matumizi
 
Uwiii Obe...Asante...Asante kwa Upendo..unaniongezea imani kubwa kuwa hapa MUNGU YUPO.NI MARA CHACHE SANA KUPATA WATU WANAOJALI NA KUTHAMINI WENGINE..NISEME UKWELI MAHALI HAPA PAMEKUA FARAJA YA PEKEE MARA ZOTE NAHITAJI KUWA NANYI NA KUSEMA NANYI JAPO NENO MOJA TU LA UPENDO..SIJAWAHI ZUNGUKWA NA UPENDO WA AINA HII WA KILA MTU KUNIJALI,KUFUATILIA,KUFAHAMU NINAVYOJISIKIA NA KUBWA KUNITAMKIA WAZI KUWA NAPENDWA..ASANTE OBE MUNGU AKUZIDISHIE KATIKA KILA HITAJI LAKO,AONGEZE UPENDO ATUSAIDIE TUONGEZE MSHIKAMANO NA UKARIMU...NAKUPENDA OBE...NAWAPENDA MAKAPUKU WOTE MBARIKIWE SANA
Mama sema neno moja tu na roho zetu zitapona
 
Kwenye mng'aro tunawapelekea watoto wanaogradueti, huku ukubwani tunaweka kwenye bahasha tu maana hatupangiani matumizi

Sloth-Laugh.gif
 
[emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji253][emoji253][emoji253][emoji253][emoji253][emoji253][emoji258][emoji258][emoji258][emoji258][emoji258][emoji258][emoji253][emoji253][emoji253][emoji253] nimemkumbuka mukongo mm jaman angekuwepo kutoa mauwa binamu Mungu anakuona kwa kunipotezea mukongo wa mama
Bora na wewe umeliona hilo
 
Back
Top Bottom